The House of Favourite Newspapers

Samatta atua Sauz kuongeza nguvu Stars

KIKOSI cha timu ya taifa, Taifa Stars kinatarajiwa kuingia nchini Lesotho tayari kwa mchezo wake wa Jumapili dhidi ya wenyeji wao hao kikitokea Afrika Kusini.

Kambi hiyo ya Stars imeno­geshwa na uwepo wa msham­buliaji na nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta, am­baye hatashiriki katika mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano lakini atashiriki katika maandalizi yote ya mchezo huo.

 

Stars iliweka kambi yake nchi Afrika Kusini kwa maandalizi ya siku 10 kuelekea mchezo dhidi ya Lesotho kwa ajili ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon).

Timu hiyo itaondoka Sauz kwa basi kwenda Maseru kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao utakaopigwa siku ya Jumapili.

 

Kocha Msaidizi wa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amesema timu inaendelea vizuri na siku ya leo (Ijumaa) itakuwa inaelekea nchini Lesotho.

“Kwa jumla timu inaendelea vizuri na maandalizi yake ya mwisho na leo Alhamisi (jana) tunafanya maz­oezi ya mwisho hapa kisha tunajiandaa kwa safari ya kesho(leo) kwenda Lesotho kwa ajili ya mechi yetu ya Jumapili,” alisema Morocco.

EXCLUSIVE: AY Afunguka “Sio Diamond tu, Hata mimi Nilishafungiwa”

Comments are closed.