The House of Favourite Newspapers

Samia: Chokochoko Zimeanza, Washajua Matumbo Yao Yanajaaje – Video

0

 

 

RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Morogoro na kupata fursa ya kuzungumza na wananchi wa mkoa huo akitokea Dodoma.

 

“Nimekuja Morogoro kwa kazi maalum ya mkutano akina mama Wakristo lakini nikasema nisimame niwasalimie, nikipata muda nitakuja kwenye ziara kwa mkoa wote wa Morogoro.

 

“Tunajua upatikanajai wa maji Morogoro, nusu wanapata nusu hawapati, Serikali inafanya jitihada za kupata vyanzo vingine vya uhakika vya maji, ili tuweze kuyasambaza kwa wananchi.

 

“Chanzo cha maji Morogoro ni Bwawa la Mindu, ambalo tumeona tope zimezidi kuliko kiwango cha maji, tumetafufa fedha ya kwenda kusafisha bwawa lile ili maji yawe mengi kuliko tope, yapikwe na kusambazwa kwa wananchi.

“Tumegundua ndani ya Morogoro maji yakipigwa kutoka kwenye bwawa kuna mabomba kupasuka kutokana na presha kuwa kubwa, sababu maji huku mwisho yanakokuja hayajaungwa kwa wingi sana. Mabomba si mabovu tatizo ni presha, maji yaliyopo yatumike.

 

“Mashamba tuliyofuta kule Kilosa yakagawiwe kwa wananchi na wawekezaji wa Sekta ya kilimo. Mashamba haya wakipewa wawekezaji yatafaa kwa kilimo kikubwa, sio vibaya kuwapa wananchi kwani watazungumza na mwekezaji kwa masharti kama ni kumpisha awekeze.

“Suala la wauza matunda (Soko la Mawenzi) mmesema lile eneo ni la Posta, tuachieni Serikali tukatazame kazi ya Posta katika eneo hilo na umhimu wa wafanyabiashara wetu, tutapima na tutaleta maamuzi ya Serikali.

“Viwanda vingi vimefungwa na tunatakiwa kuvifufua, lakini vipo vingine hata hizo mashine zilikoko huko ndani zimeshakufa. Wafufuaji huangalia soko na tija itakayopatikana, Morogoro mkilima sana mafuta, mwekezaji atatokea, kiwanda cha mafuta kitafufuka.

 

“Lile eneo ambalo lilikuwa na mgogoro la Star City, kama kuna eneo kule pimeni mtuambie Serikali, watu wanakuja kuwekeza kwenye Industrial Parks, wawekezaji wapo wengi sana, tutawaleta na watu wetu watapata ajira.

 

“Hospitali ya Wilaya ilianza kujengwa mwaka 2018 haijamalizika mpaka leo, ipo 75%, niwaombe viongozi kuweka mkazo kwenye hospitali ile ikamilike haraka, tuweke vifaa, tuweke madaktari ili ianze kutumika kama tulivyotarajia.

“Barabara za vijijini kutoka Bigwa kwenda Kisaki ni mbovu lakini tunakwenda kuongeza uwezo wa TARURA kiufundi na kifedha ili waweze kuzishughulikia haraka.

 

“Chokochoko zimeanza, msizipokee, wanaokuja na chokochoko washajua matumbo yao yanajaaje, chakula chao wanatoa wapi, pesa za matibabu watatoa wapi, wasije wakawaingiza mkenge, pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani, mkeo na watoto na msijue chakula kitatoka wapi.

 

“Niwaombe sana tutunze amani yetu, mpaka hapa tulipofika ni kwa sababu nchi yetu imetulia, zinapotokea fujo tunazikabili haraka na mambo yanakuwa shwari, tuitunze amani ya nchi yetu, tuchape kazi.” – Rais Samia Suluhu akiwa Msamvu.

 

Leave A Reply