The House of Favourite Newspapers

Samia: Tutaendeleza Mazuri Yote ya Magufuli – Video

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassana amesema Serikali yake itahakikisha inaendeleza mazuri yote yaliyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

 

Mhe. Samia ametoa maagizo hayo leo Alhamisi, Oktoba 14, 2021 wakati wa hafla ya kilele ha mwenge wa uhuru pamoja na kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Uwanja wa Magufuli, Chato mkoani Geita.

 

 

“Nawapongeza wananchi wa Chato kwa kuwa wenyeji wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu 2021 na kufanikisha kilele cha mbio hizi.

 

“Kuna baadhi ya wananchi bado hawajaacha tabia ya kuwa na mashamba ya bangi katika safu za milima na misitu, haya ni matumizi mabaya ya ardhi, pamoja na kwamba kilimo hichi kinawapatia fedha nyingi lakini hakina baraka za Mwenyezi Mungu.

 

“Madawa ya kulevya yanaathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo natoa wito kwa vijana kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya. Pia natoa rai kwa vijana kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.

 

“Serikali inajipanga kujenga Chuo cha TEHAMA hapa nchini na kikubwa Afrika Mashariki na Kati ikiwa ni kutambua mchango wa sekta hii katika uchumi na kuzalisha ajira.Tutaendeleza mambo yote mazuri yaliyoanzishwa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli yakilenga kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta zote.

 

“Mwalimu aliwajali wanyonge ambao walihitaji kukombolewa kutoka katika mazingira yasiyokuwa na haki wala huruma kwa binadamu wengine, hakika alikuwa na moyo rahimu, yeye pia aliamini kama kiongozi anahitaji kuongoza Taifa linalojitegemea.

 

“Serikali inakamilisha vigezo vya Wilaya ya Chato kuwa Mkoa. Nawakumbusha wananchi wote kuitunza na kuiendeleza miradi yote ya maendeleo iliyozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021.”

 

“Awamu zote zimekuwa zikimuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Leo sote tunawajibika kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuwa alikuwa kiongozi bora, kiongozi asiyebagua watu na aliwajali wanyonge ambao walikuwa wanahitaji kukombolewa.

 

Baba wa Taifa alisisima imara kupinga ubaguzi. Serikali itaendeleza na kudumisha mema, falsafa na itikadi na mema yote yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu Nyerere aliamini kuwa yeye kama kiongozi anahitaji kujenga Taifa linalojitegemea,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply