The House of Favourite Newspapers

Sandra Aanika Udhaifu wa Bongo Movies

0
Salama Salmini ‘Sandra’

MSANII wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’ ambaye kwa sasa ana mkataba mnono wa kucheza Tamthilia ya Nyota nchini Kenya, amesema kutokana na kufanya kazi na soko la filamu la nchini humo amegundua upungufu katika soko la Bongo ikiwemo vitendea kazi.

 

Akipiga stori na paparazi wetu, Sandra alisema miongoni mwa vitu vilivyosababisha tasnia ya filamu Bongo kuyumba ni vitendea kazi, tofauti na Wakenya wanapokuwa wanashuti wanakuwa na vifaa vingi vya kushutia na vyenye ubora.

 

“Baada ya kuanza kufanya kazi na Wakenya kuna upungufu nimeugundua, mfano huku Bongo tukishuti unakuta tunaenda na kamera mbili wakati kule wenzetu wanaweza kuwa nazo hata tano, au zaidi kazi inafanyika fasta inaisha haraka,”alisema Sandra.

Leave A Reply