The House of Favourite Newspapers

Sangoma Anaswa na Mguu wa Bundi, Mkia wa Nyumbu

0
Bundi.

 

Mganga wa kienyeji ‘sangoma’ katika Kijiji cha Majimoto kilichopo katika Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Kambona Nkana anayejulikana kwa jina maarufu la Kilosa (48) amefikishwa mahakamani baada ya kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.6

 

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alikamatwa akiwa na mkia wa nyumbu wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.4 na mguu wa bundi wenye thamani ya shilingi 248,000 ambazo alikuwa akizitumia katika kazi yake ya uganga.

 

Mshtakiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mlele, Teotimus Swai na hakutakiwa kujibu lolote kwakuwa kosa lake ni la uhujumu uchumi ambalo halina dhamana na kwamba Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kuisikiliza.

 

Awali, mwendesha mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Bakari Hongoli alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 6 mwaka huu saa kumi na nusu jioni, nyumbani kwake kijijini Majimoto wilayani Mlele.

Leave A Reply