The House of Favourite Newspapers

Sarah Azidi Kumvua Nguo Harmo

0

WAPO wanaosema kuwa wazungu wakichafukwa huwa wanachafukwa kwelikweli! Hicho ndicho kinachotokea kwa aliyekuwa mwandani wa staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’, Sarah Michelotti ambaye ni mzungu na raia wa nchini Italia.

 

Imeelezwa na watu wa karibu wa wawili hao kwamba, wiki kadhaa zilizopita baada ya kutengana kwao, bado Sarah ameendelea kumvua nguo Harmonize au Harmo akitaka amrudishie vitu alivyomsaidia wakati wa enzi za penzi lao likitaradadi.

 

Baadhi ya watu wanaamini kwamba wazungu siyo watu wa kujali vitu vidogovidogo, lakini kwa Sarah imekuwa tofauti kwani mbali na kutaka talaka yake, lakini ameapa kuchukua kila kilicho chake hata kama ni kijiko.

 

“Eti kuna watu wanasema huwa wazungu hawajali vitu vidogo kwenye mapenzi. Nani amewadanganya? Au Sarah wa Harmonize siyo mzungu?“Mbona anadai apewe kila kitu chake hata kama ni kijiko?

“Kama mmefuatilia kuna sauti ya Sarah imesambaa akimweleza Harmonize kwamba anataka amrudushie lile gari lake aina ya Audi.“Lakini mbali na hilo anataka kila kitu alichomsaidia Harmonize arudishiwe na kati ya vitu vinavyomfanya kuwa na hasira ni kuona lile gari lake (Audi) likitumiwa na mwanamke ambaye ni raia wa Ethiopia anayesemekana ndiye mwanamke mpya wa Harmonize.“

 

Sarah mwenyewe amemtumia mtu picha ya mwanamke huyo mpya wa Harmonize akiwa anatumia gari hilo.“Sasa Sarah ameapa kutinga Bongo kuchukua kila kilicho chake,” alisema mmoja wa watu wa karibu wa Harmo na Sarah aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.

 

Mbali na hayo, kuna madai kwamba, kuna fungu la pesa ambalo Sarah alikuwa akimsaidia Harmonize kwa ajili ya kushuti video za nyimbo zake na kuendeleza sanaa yake ya muziki hivyo haijafahamika kwenye hilo eneo itakuwaje.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuhusu kinachoendelea kati ya wawili hao, mmoja wa mameneja wa Harmo, Rajabu Mchopa anakiri kusoma na kusikia mambo mengi yanayosemwa, lakini akasema hayo ni mambo binafsi na kwa upande wake akaomba aulizwe mambo yanayohusiana na kazi ya msanii wake huyo.“

 

Nimesikia na kusoma huko mitandaoni, lakini naomba uniulize mambo yanayohusiana na muziki wa Harmonize kwa sababu hayo ni mambo binafsi,” anasema Mchopa. Harmo na Sarah walidaiwa kufunga ndoa ya siri Septemba 7, mwaka jana jijini Dar na kufanya sherehe iliyohudhuriwa na watu wachache jambo ambalo liliwafanya wengi kuingiwa na hisia hasi kuwa huwenda wawili hao walikuwa wanatafuta kiki.

 

Hata hivyo, kwa sasa kila mmoja anakiri kuchukua hamsini zake huku Sarah akimtolea Harmo tuhuma nzito ikiwemo ile ya kutokuwa na uwezo wa kumpa mimba mwanamke baada ya jamaa huyo kudai kuwa ana mtoto aliyekuwa akimficha.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply