The House of Favourite Newspapers

Saudia Yatoa Tende Kwa Mfungo wa Ramadhan

0
Balozi wa Saudia Arabia, Mohammed Almalik,(Katikati) akimkabidhi zawadi ya tende Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zuberi.
Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zuberi akizungumza.
Makabidhiano yakiendelea.

BALOZI wa Saudi Arabia nchini Mohammed Almalik ametoa zawadi ya tende tani 43 kwa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kwa ajili ya maandalizi ya mfungo wa Ramadhan.

Msada huo umekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam kwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zuberi, kwenye ofisi za makao makuu ya Bakwata jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari wakati akikabidhiwa Mufti aliishukuru Saudi Arabia kwa msaada huo na kwamba utasambazwa kwa taasisi zote za Kiislamu katika mikoa yote nchini.

Aliongeza kwamba tani 43 zilizoletwa zinategemewa kufikishwa tani 100 ambazo zitafika kabla ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhan.

Aidha Saudi Arabia imeahidi kuwa itakuwa inatoa msaada kila mwaka katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply