The House of Favourite Newspapers

Mauzo Hisa Yaongezeka Toka Bil 6 Wiki Iliyopita Hadi Bil 8.1 Wiki Hii

0

Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimeongezeka zaidi ya mara mbili
kutoka hisa 745,000 hadi hisa 1,878,000. Mauzo ya hisa yameongezeka pia
kutoka Shilingi Bilioni 6 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 8.1 wiki hii.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
TBL       ………………….96.33%
CRDB  …. ………………..2.43%
DSE      ……………………0.54%

Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umeongezeka kwa
Shilingi  Billioni 38 kutoka Shilingi Trilioni 20.248 wiki iliyopita hadi
Shilingi Trilioni 20.286 wiki iliyoishia tarehe 12 Mei 2017. Hii ni kutokana
na kuongezeka kwa bei za hisa za NMG (18.37%), DSE (9.09%) na KCB (5.8%).
Mtaji wa kampuni za ndani umeshuka kwa Shilingi Bilioni 141 kutoka Shilingi
Trilioni 7.351 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.210 wiki hii. Hii ni
kutokana na kushuka kwa bei ya hisa za TBL (-4.35%).

Viashiria (Indices)

Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimeongezeka
kwa pointi 4.3 kutoka pointi 2,327 hadi pointi 2,332 kutokana na kuongezeka
kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.

Kiashiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimeshuka kwa pointi 67 kutoka
pointi 3,497 wiki iliyopita hadi pointi 3,430 wiki hii.

Sekta ya viwanda (IA) imeshuka kwa pointi 130.79 kutoka pointi 4,489 wiki
iliyopita hadi pointi 4,358 wiki hii kutokana na kushuka kwa bei ya hisa za
TBL kwa asilimia 4.35%.

Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imeongezeka kwa pointi
8.11 kutoka pointi 2,543 hadi pointi 2,552 kutokana na kupanda kwa bei ya
hisa za DSE kwa asilimia 9.09%.

Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye
wastani wa pointi 3032 imetokana na bei ya hisa za SWISSPORT kubaki kwenye
shilingi 5150

Hati Fungani (Bonds)
Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 12 May 2017 yameshukaka
kutoka thamani ya Shilingi Bilioni 27.1 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni
22.61 wiki iliyoishia 12 Mei 2017.
Hii ilitokana na mauzo ya hati fungani kumi na nne (14) za serikali zenye
jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 31.45 kwa jumla ya gharama ya Shilingi
Bilioni 22.61.

Tunaendelea kuhamasisha wanafunzi waendelee kujisajili kwenye shindano letu
la Scholar Investment Challenge kupitia leverage scholar app au tovuti
www.younginvestors.co.tz

Leave A Reply