The House of Favourite Newspapers

Savara Aachia Albamu Yake Ya ‘Savage Level’

0
MSANII kutoka Kundi la Sauti Sol la nchini Kenya, Savara ameachia albamu yake aliyoipa jina la Savage Level sambamba na kutambulisha ngoma nyingine kutoka katika albamu hiyo iitwayo Sababisha.
Albamu hiyo ya Savara ina jumla ya nyimbo 14 ambazo zote ameziandaa na ‘kuziprodyuzi’ mwenyewe, zikiwa na mchanganyiko wa maudhui mbalimbali katika jamii ikiwemo mapenzi, elimu ya kiroho, ukuaji, matatizo ya msongo wa mawazo na kadhalika.
Kabla ya kuachia albamu hiyo, tayari Savara tayari alishaanza kufanya poa kama solo artist nje ya Kundi la Sauti Sol baada ya kuachia ngoma kama Balance na Killem Everybody ambazo zimepokelewa vyema ndani na nje ya Afrika Mashariki.
Katika albamu yake hiyo, Savara ameshirikiana na wasanii Karun kwenye wimbo wa Vibration na Nyashinski katika ngoma ya More Than A Friend huku akielezea kwamba kilichomsukuma kuandika ngoma yake ya Sababisha, ni jinsi uhusiano wake na mama yake ulivyokuwa tangu alivyomzaa na jinsi alivyohangaika kumlea mpaka kuwa mtu mzima.
Akiingumzia albamu ya Savage Level, Savara amesema: “Hii ni zaidi ya chakula cha ubongo, inakupa nguvu ya kubadilisha mtazamo wa maisha yako kwenda kwenye uhalisia. Kila mmoja anazo nguvu ndani yake ambazo zinaweza kumfanya kuwa mtu bora, katika albamu hii nimejaribu kumuonesha kila mtu namna ya kuzifikia nguvu hizo.”

Leave A Reply