The House of Favourite Newspapers

SBL Yashirikiana Na Usalama Barabarani, Polisi Jamii CUP Kukuza Kunywa Kwa Uwajibikaji Na Usalama Barabarani

0
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ramadhani Ng’anzi akisalimiana na Bondia Karim Mandonga baada ya uzinduzi wa Kamanda CUP.

Dar es salaam, 12 Oktoba – Mwanamasumbwi mwenye tambo nyingi, Karim Mandonga na Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature a.k a Sir Nature ni miongoni mwa mabalozi watakaohamasisha michuano ya Kamanda Cup iliyozinduliwa na Kampuni ya Serengeti Breweries Limited kupitia chapa yake ya Serengeti Premium Lager.

Kampuni hiyo inafurahi kutangaza ushirikiano wake na Polisi wa Trafiki wa Tanzania kwa USALAMA BARABARANI JAMII CUP 2023, mashindano maarufu ya mpira wa miguu yanayojumuisha waendesha pikipiki. Ushirikiano huu unawakilisha hatua kubwa katika azma ya Serengeti Breweries Limited ya kukuza elmu juu ya kunywa kwa uwajibikaji na usalama barabarani katika jamii yetu kupitia kampeni yao chanya ya kunywa inayoitwa ‘INAWEZEKANA’.

Kamanda wa Kikosi Cha usalama barabarani nchini, SACP. Ramadhani Ng’anzi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya INAWEZEKANA kwa kushirikiana na SBL inayolenga kutoa elimu na kuhamasisha watu kutotumia vile na kuendesha vyombo vya moto, katika ukumbi wa Police Mess, jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza kushoto kwake ni Mwanasheria Mkuu wa Kikosi Cha usalama barabarani, SSP Deus Sokoni na kulia ni Mkurugenziwa masoko wa Serengeti Breweries limited, Anitha Msangi ambapo kampeni hiyo ilizinduliwa pamoja na mashindano ya ‘USALAMA BARABARANI POLISI JAMII CUP’.

Lengo kuu la Serengeti Breweries Limited katika Kampeni ya INAWEZEKANA ni kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa tabia chanya za kunywa vilevi, na kusisitiza kwa juu ya kujizuia na dhana kwamba kunywa kwa uwajibikaji kunahakikisha usalama, afya, na ustawi.

USALAMA BARABARANI POLISI JAMII CUP, inayojulikana kwa kujitolea kwake kwa waendesha pikipiki, inatoa jukwaa bora la kufikia sehemu muhimu ya jamii yetu. Serengeti Breweries Limited inajivunia kuungana na jeshi la polisi idara ya usalama wa barabaran ya Tanzania kukuza kunywa kwa uwajibikaji na usalama barabarani.

Kupitia ushirikiano huu, Serengeti Breweries Limited inalenga kushirikisha waendesha pikipiki na wapenzi wa mpira wa miguu katika ngazi zote za mashindano, kuanzia kwenye ngazi za kata hadi kitaifa.

Anitha Rwehumbiza, Mkurugenzi wa Ubunifu na Masoko wa Serengeti Breweries Limited alisema, “Serengeti Breweries Limited inaamini kwa dhati kuwa kunywa kwa uwajibikaji kunaanzia na kila mtu binafsi. Inahusisha kufanya chaguo sahihi kuhusu matumizi ya pombe na kuelewa matokeo makubwa ya matendo ya mtu kwenye barabara na katika jamii. Kampeni ya INAWEZEKANA inalenga kukuza na kuhamasisha tabia za kunywa kwa uwajibikaji na usalama barabarani ndani ya jamii yetu.”

Mkurugenzi wa Mawasilino wa SBL John Wanyancha akizungumza kwenye uzinduzi huo.

“Tuna furaha kushirikiana na POLISI JAMII CUP kwani inawiana na maono yetu ya kuhakikisha usalama wa wateja wetu. Mashindano haya yanajumlisha jukumu kubwa katika kuongeza uelewa kuhusu kunywa kwa uwajibikaji na kuwaelimisha Watanzania kwa ujumla kuhusu njia tofauti za kuepuka uendeshaji wa gari wakiwa wamelewa.

Hii sio mara ya kwanza kushirikiana na polisi wa trafiki nchini Tanzania; tumefanya hivyo hapo awali kufikia wateja wetu na madereva wa magari katika mikoa tofauti kama Dar es Salaam, Mwanza, Iringa, na Dodoma,” alihitimisha Bi. Rwehumbiza.

Ramadhani Ng’anzi, Kamanda wa Idara ya Trafiki ya Tanzania, alisema, “Idara ya Trafiki, kupitia USALAMA BARABARANI POLISI JAMII CUP na Serengeti Breweries Limited, inalenga kukuza usalama barabarani, kwa kudhibiti uendeshaji wa gari wakiwa wamelewa. Ushirikiano huu unaendana na lengo letu la kuwahamasisha waendesha pikipiki na madereva wote kufuata sheria za barabarani na kuendesha kwa usalama.

Wadau wakiwa na viakisi mwanga baada ya kukabidhiwa kwenye uzinduzi huo.

Kupitia njia ya kipekee ya kutumia mpira wa miguu, mashindano haya yanajumlisha waendesha pikipiki kushindana kutoka ngazi za kata hadi kitaifa, na kusaidia kuibua vipaji vya mpira wa miguu. Tuna dhamira kubwa ya kufanya barabara zetu kuwa salama zaidi kwa kukuza tabia za kunywa kwa uwajibikaji, na tunatarajia kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo haya.”

Kampeni ya INAWEZEKANA inaonesha dhamira kuu ya Serengeti Breweries Limited katika jukumu lake la kijamii na ustawi wa wateja wake na jamii kwa ujumla. Pamoja na KAMANDA CUP, Serengeti Breweries Limited inalenga kujenga utamaduni wa kunywa kwa uwajibikaji na usalama zaidi.

Kuhusu SBL:

Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za biazilichukua nafasi ya Zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo.SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji iliyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingina EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za ajirakwa watu wa Tanzania.

Chapa za SBL zimepokea tuzo nyingi za kimataifa zikiwemo Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Guinness Stout, naGuinness Smooth. Kampuni hii pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnniew Walker Whisky, Smirnoff Vodka,Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum, Baileys Irish Cream, na chapa zinazozalishwa nchini kama vile Bongo Don SBL’S maiden localspirit brand na Smirnoff Orange. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Rispa Hatibu,

Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL,

Simu: +255 685 260901

Barua Pepe: [email protected]

Leave A Reply