The House of Favourite Newspapers

Sean Kingstone Ashtakiwa kwa Kushindwa Kulipa Cheni

0

MWANAMUZIKI kutoka Jamaica, Kisean Paul Anderson ambaye anafahamika zaidi kama Sean Kingston, mwenye makazi yake Marekani, anaendelea kuandamwa na majanga baada ya  kushtakiwa na muuzaji mmoja wa vito vya thamani kwa kushindwa kulipa fedha ya cheni hiyo.

 

Tovuti ya TMZ imeripoti kwamba rekodi za mahakama zinaonesha kwamba Kingston alifikishiwa mzigo huo lakini hadi leo bado hajafanya malipo.

 

Kumbukumbu zinaonesha kwamba hii imekuwa tabia ya mwimbaji huyo, mwaka 2017 alishtakiwa kwa kushindwa kulipia gari alilouziwa, miezi michache baadaye muuzaji wa vito vya thamani alimshtaki kwa kushindwa kulipa deni la Saa aina ya Rolex, alishindwa kesi hiyo na alitakiwa kumlipa muuzaji huyo ($300K) takribani TSH. 695M.

 

Kingstone mwenye miaka 30, anakumbukwa kwa vibao vyake vikali kama “Beautiful Girls”, “Fire Burning”, na “Eenie Meenie”.

Leave A Reply