The House of Favourite Newspapers

Sehena ya Dozi 499,590 za Pfizer Yatua Tanzania

0


Serikali ya Tanzania imesema leo Novemba 23, 2021 Tamzania imepokea Dozi 499,590 za Pfizer kutoka nchini Marekani ambazo zitakinga Watanzania 249,795 (dozi mbili), Chanjo hizi za Pfizer ni kama zilivyokuwa za Janssen na Sinopharm zimethibitishwa na WHO kuwa ni bora na salama.

 

“Hadi kufikia November 19,2021, takwimu zinaonesha kuwa wananchi 1,359,624 walipata chanjo, nitoe pongezi zetu za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali Taifa letu na kutuletea huduma hii ya chanjo dhidi ya UVIKO-19.

 

“Ninawaagiza Viongozi na Watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaelimishwa kwenda kupata chanjo ili kujikinga dhidi ya UVIKO-19,” amesema Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima wakati wa upokeaji wa chanjo Dar es salaam.

Leave A Reply