The House of Favourite Newspapers

Selasini: Mimi ni Mwanachama Halali wa NCCR-Mageuzi, Ashangazwa na Chadema – Video

0
Mwanasiasa mkongwe Joseph Selasini amesema yeye ni mwanachama halali wa NCCR-Mageuzi

MWANASIASA mkongwe Joseph Selasini amesema yeye ni mwanachama halali wa NCCR-Mageuzi na hana uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

 

Selasini ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari huku akibainisha kuwa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Siasa kifungu namba 8A (2) (C) na kifungu namba 8C (1) (C) kinakitaka kila chama cha siasa kupeleka katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa orodha ya majina ya Wajumbe wa Kamati Kuu, Wajumbe wa Halmashauri Kuu, Wajumbe wa Baraza Kuu na Wajumbe wa Mkjutano Mkuu hivyo ni vyema kwa yeyote aliye na mashaka na uanachama wake aende akafanye utafiti athibitishe kama jina lake lipo au halipo.

 

Kwa upande mwingine Selasini amebainisha kuwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi uliofanyika Mei 21 ulikuwa ni mkutano halali ambao ulikuwa na jumla ya wajumbe 52 na kwa mujibu wa Katiba ya NCCR-Mageuzi Mkutano wa Halmashauri Kuu unakuwa na jumla ya wajumbe 82, ili mkutano uweze kufanyika lazima uwe na nusu ya idadi ya wajumbe wanaotakiwa kuwepo kwenye mkutano huo, hivyo kwa muktadha huo mkutano ule ulikuwa halali.

Joseph Selasini ameongea na waandishi wa habari juu ya sakata linaloendelea ndani ya Chama cha NCCR-Mageuzi

Selasini amesema hoja ya kuwa mkutano ule ulikuwa na wajumbe feki ni hoja ya uongo kwani wajumbe hao waliandika majina yao na nafasi zao lakini pia walirekodiwa katika kumbukumbu maalum.

 

Akiongea na waandishi wa habari Selasini amesisitiza kuwa katika kikao kile Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi wa Zanzibar alikuwepo na ndiye aliyeshinikiza kikao kiendelee.

Leave A Reply