The House of Favourite Newspapers

SEMI TRAILER LAVAMIA DUKA, WATATU WANUSURIKA KIFO

lori hilo baada ya kuvamia duka.

 

WATU watatu wamenusurika kifo mjini Morogoro baada ya kutokea ajali mbaya ya lori la mizigo, (Semi Trailer) ambalo dereva wake ameshindwa kulimudu na kuparamia duka la dawa za binadamu.

 

Mashuhuda wakitaharuki.

 

Tukio hilo limetokea leo mchana, Jumatatu Machi 19, 2018 katika Mtaa wa Nguzo, Kata ya ya Mazimbu eneo linalofahamika kama Ipoipo baada ya dereva wa lori hilo mwenye asili ya Kiarabu kufanya uzembe wakati akiendesha.

 

 

Hali ilivyokuwa eneo la tukio.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamedai gari hilo ambalo ni mali ya kampuni ya baba yake ijulikanayo kama AA. TRANS LIMITED, alikuwa akiliendesha kwa mbwembwe akitokea maeneo ya Tumbaku kuelekea Kihonda Maghorofani lilipomshinda na kusababisha ajali hiyo.

 

Walionusurika ni dereva wa lori hilo (jina lake halijajulikana) aliyeumia kichwani na mikononi, muuza duka la dawa, Joyce Mwene, aliyeumia mkononi na begani.

Dereva wa lori akiokolewa.
Lori hilo likitolewa.

 

Mwingine ni dereva wa gari dogo aina ya Toyota Noah aliyenusurika baada ya gari lake kukwanguliwa na kupasuliwa vioo vitatu huku yeye akitoka salama.

 

 

Jeshi la Polisi mkoani Mororgoro linamshikilia dereva wa lori hilo kwa mahojiano zaidi ambapo kwa sasa amepelekwa hospitali chini ya ulinzi wa polisi.

Na dustan Shekidele | Global Publishers.

Comments are closed.