The House of Favourite Newspapers

Semina Ya Fursa Dar: Mbinu Lukuki za Kujikwamua Zatolewa kwa Washiriki

fursa-6Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akitoa somo kwa wanasemina waliohudhuria.

fursa-2Umati wa watu waliohudhuria semina hiyo.

fursa-3

fursa-4Kutoka kushoto ni wahamasishaji wa semina hiyo, wasanii Nick wa Pili, Mrisho Mpoto na wengine.

fursa-14

Ruge akizidi kufunguka.

fursa-1 fursa-5  fursa-7 fursa-8 fursa-9 fursa-10Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ (wa pili kutoka kushoto) akifuatilia semina hiyo.fursa-11 fursa-12 fursa-13

MAMIA ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam leo wamejitokeza kwenye semina ya kufahamu mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi kupitia elimu ya ujasiriamali, biashara na mambo mengine kupitia kwa wahamasishaji, Nikki wa Pili, Ruge Mutahaba, Richard Kasesela, Rose Urio na Mkurugenzi Mtendaji wa MaxCom Africa, Juma Rajab kwenye Ukumbi wa Milenium Tower (LAPF) Kijitonyama.

Akizungumza katika semina hiyo, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, ambao ndio waandaaji, Ruge Mutahaba, alisema kupitia semina hiyo maarufu kwa jina la ‘Fursa 2016 Ongeza Thamani’ iliyofanyika kwenye mikoa mbalimbali nchini, wamewapatia vijana mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia rasilimali zilizopo nchini.

Amesema tatizo kubwa lililopo miongoni mwa vijana ni kutokutenga muda wao vizuri kwani wanautumia muda mwingi kufanya vitu visivyokuwa na manufaa ya baadaye huku akitumia mfano vijana wengi kutumia muda wao katika matumizi ya mitandao ya kijamii na mambo mengine yasiyokuwa na manufaa.

Alieleza kuwa, waajiri wanapaswa kuwapa kazi nyingi wafanyakazi wao ili kuweza kuondokana na dhana ya kuwa wafanyakazi wao wasipoteze muda kwenye mitandao ya kijamii.

“Hili ni tatizo kubwa, vijana wengi wamekuwa wakipoteza muda sana kuperuzi mitandaoni. Niwashauri waajiri pia, kwenda nao sambamba kwa kuhakikisha wanawapa kazi nyingi ili wakose muda wa kuperuzi na waendane na kasi ya  serikali yetu ya Awamu ya Tano,” alisema Ruge.

Vilevile alieleza namna vijana wanavyoweza kubadilisha mitindo yao ya maisha ya kila siku kwa kufikiria kuwa serikali inaposema inahitaji watu wasonge mbele kimaendeleo haimaanishi kwamba hayo maendeleo yatakuja tu ukiwa haujishughulishi, lazima ufanye kazi kwa bidii na mafanikio utayaona.

rap

Comments are closed.