The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Sentensi 26 za Rais Magufuli Leo Aprili 12, 2017

0

RAIS Dkt John Pombe Magufuli, leo Aprili 12, 2017 ameweka Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Kimataifa ambayo treni ya kisasa inayotumia umeme itaweza kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Viwanja vya Pugu, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Rais Magufuli ameeleza haya;

  1. Nataka mkandarasi ajitahidi amalize mradi huu kabla ya miezi 30, ikiwezekana siku ya uzinduzi watu wapande bure hadi Dodoma wakashuhudie sherehe ya ofisi za serikali kuhamia Dodoma.
  2. Reli ya kisasa itarahisisha usafiri na usafirishaji wa mizigo nchini na nchi jirani za DRC, Rwanda, Burundi, Uganda.
  3. Ujenzi wa reli hiyo utakuza biashara miongoni mwa nchi zinazotuzunguka, ambapo kikwazo kikubwa kwa sasa ni miundombinu mibovu.
  4. Reli hii itakuza sekta za viwanda, Kilimo, Mifugo na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa viwandani na kwenye masoko.
  5. Treni ni njia ya bei nafuu na salama zaidi kusafirisha mizigo. hivyo tutaokoa fedha zetu ambazo hutumika kukarabati barabara.
  6. Reli itatoa ajira nyingi, wakati wa ujenzi itatoa ajira takribani laki 6, ikikamilika ajira milioni 1 kwenye za sekta mbalimbali
  7. Reli hii ya kisasa itahusisha pia ujenzi wa stesheni 6 na bandari kavu eneo la Ruvu ili kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam.
  8. Fedha za ujezi wa reli zilitengwa tangu mwezi Julai mwaka jana (2016) lakini hatukuweza kumpa mkandarasi hadi atakapoanza ujenzi huo.
  9. Rais wa Uturuki amekubali kutupa mkopo wa kujenga reli hii kutoka Morogoro hadi Dodoma na tayari ametuma wawakilishi
  10. Wale wataalam wa kusoma kwenye mitandao, wakasome nchi gani imejenga reli hii kwa fedha za ndani, ni Tanzania tu.
  11. Ukiwa dereva wa lori, hutakiwa kusikiliza watu uliowapakia wanaimba nini au wanatazama wapi, wewe endesha lori uwafikishe salama
  12. Mimi ni dereva mzuri na kwenye lori langu kuwa wanaoimba, wanaotazama nyuma, waoongea, lakini nitalifikisha ninapotaka lifike.
  13. Dereva mzuri huwa hasikilizi watu aliowapakia wanasema nini, haangalii kule wanapoangalia wao. Hili lori la maendeleo litafika.
  14. Tunajua tunapokwenda, mtu asitake kubadilisha ajenda yetu tuanze kuzungumzia mambo ambayo hayapo kwenye ilani ya chama.
  15. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi, sasa mtu amekaa kwenye ufisaidi miaka 50, huyo ni mbichi tena?
  16. Fisadi mkunje angali mbichi, akikomaa mvunje. Na wakati wa kumvunja lazima atalalamika
  17. Ninayoyafanya ni kwa niaba yenu Watanzania. Nilipozuia mchanga, sikushindwa kuwaambia na mimi wanipelekee makontena mawili Ulaya.
  18. Mimi ninawaambia Watanzania, siku moja mtaikumbuka awamu ya tano sababu ni awamu ya kazi.
  19. Tanzania ni tajiri sana, hatupaswi kuwa ombaomba lakini tumechezewa sana. Nasema inatosha tutasonga mbele
  20. Ujenzi wa reli utasaidia kutunza barabara zetu. Barabara nyingi zinaharibika sababu ya kusafirisha mizigo mikubwa.
  21. Nchi za Afrika zinachonganishwa na watu wasiojulikana halafu wanapigana wenyewe kwa wenyewe badala ya kupigania maendeleo.
  22. Nchi za Afrika zinachonganishwa na watu wasiojulikana halafu wanapigana wenyewe kwa wenyewe badala ya kupigania maendeleo.
  23. Viongozi wa vyama vya siasa, acheni CCM ifanye kazi, tukakutana 2020 lakini sasa ni kazi tu.
  24. Hapa naona mmeandika spidi itakuwa ni 160km/h, hata mkitaka fanyeni 180km/h sababu Watanzania wanapenda spidi wafike haraka.
  25. Mimi ni dereva mzuri na kwenye lori langu kuna wanaoimba, wanaotazama nyuma, wanaoongea, lakini nitalifikisha ninapotaka lifike.
  26. Niwaagize wahusika, ujenzi wa Reli ya kisasa ya Dar- Morogoro utakapoanza, ajira zote wapewe wakazi wa Pugu.

Baada ya kuweka jiwe la msingi, Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Pugu waliojitokeza, na kisha kuondoka” – JPM

Leave A Reply