The House of Favourite Newspapers

Senzo: Msiwe na presha, Tunachukua Pointi

0

MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha, amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo kuelekea kwenye
mchezo wa Ligi
Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa leo Jumamosi, Uwanja wa
Mkapa huku akiweka
bayana wataibuka na pointi tatu.


Yanga inayonolewa na Kocha
Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kariakoo
Dabi ukiwa mchezo wa kwanza
kukutana kwa msimu huu kwenye ligi.


Akizungumza na
Championi Jumamosi, Senzo alisema kuwa haipaswi kwa mashabiki wa timu hiyo kuwa na presha
na timu yao kwa kuwa
ina wachezaji wazuri na mechi zote kwenye ligi ni sawa.


“Hakuna sababu ya kuwa na
presha unajua mchezo wetu wa ligi dhidi ya Simba ni sawa na mechi nyingine ambazo tumecheza.


“Kuelekea katika mchezo wetu
dhidi ya Simba, tunahitaji kuona tunapata matokeo mazuri ili tuweze
kushikilia ambapo tupo.


“Utakuwa mgumu kulingana na
ukubwa wa mchezo husika, huu ni mchezo mkubwa kwa Afrika, hivyo
hata sisi viongozi tunauchukulia
katika ukubwa huo, ndio maana tunatamani kuwa washindi,” alisema Senzo.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA NA MARCO MZUMBE

Leave A Reply