The House of Favourite Newspapers

Serikali Kenya Yamlinganisha Odinga na Alshabaab, Al Qaeda

Serikali ya Kenya kupitia kwa Waziri wa Usalama, Dkt Fred Matiang’i,  imelipiga marufuku kundi la National Resistance Movement (NRM) lililo chini ya Muungano wa Upinzani (NASA) nchini humo na kulitangaza kuwa ni kundi la kihalifu.

Kundi hilo limeundwa baada ya Raila Odinga kususia uchaguzi wa marudio na limekuwa katika harakati za kutaka mabadiliko katika uchaguzi na kuwashawishi wananchi kususia bidhaa za makampuni ambayo yanadiwa kuwa upande wa serikali ya nchi hiyo.

 

 

Aidha, waziri huyo ameliweka kundi la NRM kwenye ordha moja na makundi ya kigaidi ya Al Shabaab na Al Qaeda ambapo hatua hii imekuja ikiwa ni baada ya Raila Odinga kujiapisha kama Rais wa Watu wa Kenya.

Ifuatayo ni taarifa ya rasmi ya serikali kulitangaza NRM kuwa kundi la kihalifu:

 

MAKUNDI MENGINE YALIYOTANGAZWA KUWA NI YA KIHALIFU NCHINI HUMO:

1. Al-Shabaab

2. Amachuma

3. Angola Msumbiji

4. Banyamulenge

5. Baghdad Boys

6. Charo Shutu

7. Chinkororo

8. Coast Housing Land Network

9. Congo by Force

10. Dallas Muslim Youth

11. Forty Brothers

12. Forty-two Brothers

13. Jeshi la Embakasi

14. Jeshi la Mzee

15. Jeshi la King’ole

16. Japo Group

17. Kamjesh

18. Kamukunji Youth Group

19. Kaya Bombo Youth

20. Kenya Youth Alliance

21. Kosovo Boys

22. Kuzacha

23. Makande Army

24. Mombasa Republican Council

25. Mungiki Movement, Mungiki Organisation, Mungiki Sect

28. Republican Revolutionary Council

29. Sabaot Land Defence Force

30. Sakina Youth

31. Sungu Sungu

32. Siafu

33. Taliban

 

CREDIT: Matiang’i declares NRM criminal group

Comments are closed.