The House of Favourite Newspapers

Serikali Kuanzisha Mkoa Mpya wa Kipolisi Rufiji

0

Serikali inatarajia kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi rufiji mkoani Pwani ili kusogeza huduma ya kipolisi karibu zaidi na wananchi na kurejesha amani na utulivu katika maeneo hayo na wilaya ya Mafia nayo itakuwa ndani ya mkoa huo mpya.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba amelieleza Bunge leo Jumanne katika hutoba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017 /18.

Nchemba amesema Mkoa huo utaitwa Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji ambao utajumuisha wilaya za Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mafia ili kuimarisha usalama katika maeneo hayo. 

Hii itasaidia kupungua kwa matukio mbalimbali ya mauaji ambayo yamegharimu maisha ya baadhi ya wananchi.

Leave A Reply