Serikali Yazindua Mpango wa “Silicon Zanzibar” kwa kushirikiana na Wasoko
Mji wa Fumba, Zanzibar, 30 Agosti 2022—Serikali ya Zanzibar jana imetangaza uzinduzi wa Silicon Zanzibar, mpango mpya wa kuvutia na kukaribisha makampuni ya teknolojia kutoka barani Afrika kuingia kisiwani humo.
Silicon Zanzibar itaboresha utoaji wa vizaza kazi kwa wafanyakazi wenye ujuzi wa teknolojia kutoka barani Afrika na kwingineko ili kuhamia Zanzibar. Serikali pia itatoa motisha kwa kampuni zinazoshiriki chini ya mpango uliopo wa Ukanda Huru wa Kiuchumi wa Zanzibar, ambao unajumuisha msamaha wa kodi ya mapato kwa kampuni kwa miaka kumi.
Kampuni za teknolojia barani Afrika zilipokea zaidi ya $6B katika ufadhili mnamo 2021, kwa tasnia ambayo imekuwa inakua kwa kasi zaidi barani.
Katika kuadhimisha uzinduzi wa Silicon Zanzibar, kwenye mkutano rasmi na waandishi wa habari utafanyika leo katika jengo la The Pavilion kwenye mji wa Fumba na kuhudhuriwa na watu mashuhuri akiwemo Waziri wa Uwekezaji na Maendeleo ya Uchumi Zanzibar, Mudrick Soraga, Waziri wa Uchumi wa Bluu na Uvuvi, Suleiman Masoud, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Harusi Suleiman, Mkuu wa Wilaya ya Unguja Magharibi, Hamida Mussa Khamis na Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Shariff Ali Shariff.
Katika kuitikia fursa hiyo, Waziri wa Uwekezaji na Maendeleo ya Uchumi Zanzibar, Mudrick Soraga alisema, “Makampuni ya teknolojia hayata hitaji tena kufungua ofisi na kuhamisha watu wao kwenda Dubai au London kusimamia shughuli zao barani Afrika.
Tunatoa mazingira ya wazi na wezeshi kwa makampuni yote ya teknolojia na washiriki wa timu zao kuwa mjini Zanzibar mojawapo ya maeneo yanayovutia zaidi duniani kuruhusu kila mtu anayefanya teknolojia kwaajili ya Afrika kuwa na msingi barani humu.”
Silicon Zanzibar inaunga mkono mojakwamoja sera ya serikali ya Uchumi wa Bluu ili kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa kupitia chini ya mazingira na mahitaji ya rasilimali endelevu. Wafanyabiashara wa kiteknolojia wanauwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi hasa kiuchumi kwa vile hawategemei hali ya hewa, jambo ambalo litaisaidia Zanzibar katika kuinua uchumi wake dhidi ya sekta za msimu kama vile kilimo na utalii.
Kuelekezea wafanyakazi wa kiwango cha juu wa teknolojia pia kutachangia kodi kwa kiasi kikubwa Zanzibar kwa kupitia mapato yao na nguvu ya matumizi ya ndani huku wakipata ujuzi na uzoefu wao na wafanyakazi wa ndani wa Tehama.
Eneo halisi la Silicon Zanzibar litapatikana katika Mji wa Fumba, kituo kikuu cha maendeleo cha kampuni ya uhandisi ya CPS ya Ujerumani, ambayo imejenga maelfu ya nyumba za kisasa za makazi na biashara kwenye ufukwe wa bahari wa kilomita 1.5 katika pwani ya kusini magharibi ya Zanzibar, umbali wa kilomita 9 tu kutoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Mkurugenzi Mtendaji wa CPS, Sebastian Dietzold alisema “CPS inasaidia kuendeleza jumuiya zenye nguvu zinazoongeza thamani kwa wawekezaji kama vile Wasoko, kwa madhumuni ya msingi ya kuwawezesha watu wa Zanzibar na wafanyabiashara”.
Silicon Zanzibar tayari imevutiwa na kampuni ya Wasoko kama mshirika wake wa kwanza, ni kampuni inayokua kwa kasi barani Afrika kama inavyotambuliwa na Financial Times, imetangaza kufungua kituo kipya katika Mji wa Fumba sambamba na kuwatumia zaidi yawafanyakazi 40 wa teknolojia na viongozi wakuu akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Wasoko, Daniel Yu.
Akizungumzia mtazamo wake juu ya uamuzi wa kuanzisha kitovu kipya, Yu alielezea, “Kama kampuni ya teknolojia ya ukanda wa African, Wasoko imekuwa ikitafuta maeneo ambapo tunaweza kuleta pamoja vipaji bora kutoka barani kote na zaidi ili kuvumbua na kukuza bidhaa mpya na huduma kwa wateja wetu.
Tunayo heshima kuwa mshirika mwanzilishi wa Silicon Zanzibar, na tunatarajia Wasoko kuwa wa kwanza kati ya kampuni nyingi za teknolojia kuanzishwa kwa uwepo katika kisiwa hiki. Waziri Soraga alimalizia kwa kusema, “Tunafuraha kuungana rasmi na Wasoko na makampuni mengine ya teknolojia yanayokuja Zanzibar ili kuunda sera na mipango itakayoibadilisha Zanzibar kuwa kituo kikuu cha teknolojia kwa Bara la Afrika.