The House of Favourite Newspapers

Shahidi Aeleza Alivyotishiwa Bastola na Sabaya

0

SHAHIDI wa nane wa Jamuhuri katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Magdalena Mallya(32) leo ameieleza Mahakama kuwa alitishiwa kwa bastola na Sabaya alipomfuata kumuomba amuachie mume wake Bakari Msangi aliyekuwa amemteka.

 

Akihojiwa na jopo la mawakili sita wa utetezi Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo shahidi huyo amesema pia baada ya Msangi ambaye ni Diwani wa CCM kata ya Sombetini baada ya kuachiwa alikuwa na damu masikioni kutokana na kipigo.

 

Amesema wakati akiwa ametekwa Msangi alikuwa amefungwa pingu na kamba miguuni na alipofika hoteli ya Tulia, Sabaya aliruhusu wazungumze akiwa chini ya ulinzi. Akihojiwa na wakili Edmund Ngemela shahidi huyo amesema baada ya kutishiwa kwa bastola na kutukanwa aliripoti polisi.

 

Sehemu ya mahojiano ilikuwa hivi.

Wakili: Unasema Sabaya alikutisha na bastola mdomoni.
Shahidi: Ndio.
Wakili: Pia alikutukana.
Shahidi: Ndio.

 

Wakili: Je, ni makosa alifanya.
Shahidi: Ndio.

 

Wakili: Je uliripoti polisi.
Shahidi: Ndio.
Wakili: Unafahamu hilo sio shitaka lilipo hapa mahakakamani.
Shahidi: Sifahamu.

Wakili: Ulipotoa maelezo hapa mahakamani ulikiwa unaelezea shitaka la kutishwa
Shahidi: Ndio
Wakili: Utajisikiaje ukiambiwa hilo shitaka halipo mahakamani.
Shahidi: Nitajisikia vibaya.

Leave A Reply