The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Wawili Wafariki kwa Kugongwa na Gari Dar

0

WATU wawili ambao ni wanafunzi wamefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Scania wakiwa stendi maeneo ya Afrikana barabara ya Bagamoyo Wilaya ya Kinondoni.

 

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Agosti 9, 2021 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro imeeleza kuwa ajali hiyo imetokea alfajiri saa 11:15 alfajiri ambapo dereva alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea.

 

“Wanafunzi waliofariki ni Collins Obed Ngowi (15) kidato cha pili Shule ya Sekondari Makongo na Salvina Otieno anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 10-15 mwanafunzi wa darasa saba Shule ya Msingi Mount Sery” imesema taarifa ya Muliro.

 

Kamanda Muliro amesema mwanafunzi mwingine Ashura anayesoma kidato cha tano shule ya Sekondari Al-Haramain alipata alijeruhiwa sehemu za mwili na kuwahishwa hospitalini, ambapo jeshi la polisi linaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo pamoja na ukaguzi wa gari hilo.

 

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum linamtaka dereva huyo ajisalimishe haraka iwezekanavyo kituo chochote cha Polisi kilicho karibu na yeye kwani hana uwezo wa kujificha zaidi ya saa 48,” imeeleza taarifa hiyo.

Leave A Reply