The House of Favourite Newspapers

Shamimu Mwasha, Mumewe Warudishwa Segerea Tena – Video

UPANDE wa mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi inayomkabili Blogger, Shamim Mwasha (41) na mumewe, Abdul Nsembo (45) bado haujakamilika hivyo umeiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kusikilizwa.

 

Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon, mbele ya Hakimu Mkazi, Janeth Mtege, wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa. Wankyo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo anaomba ahirisho la kesi hiyo.

 

Hakimu Mtega ameiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 6 mwaka huu na washtakiwa wamerudishwa rumande. Washtakiwa wanatuhumiwa kukutwa na kusafirisha dawa za kulevya, Mei 1, 201 kinyume cha sheria.

 

Comments are closed.