The House of Favourite Newspapers

Shamsa Ford na Chid Mapenzi: Kutoka Kwenye Ndoa Mpaka Kaka na Dada

0

Shamsa Ford mwanadada mrembo kwenye tasnia ya uigizaji na mfanyabiasha wa nguo za kike hasa madira na vijora, mwaka 2016 aliingia katika mahusiano ya kimapenzi na mfanyabiasha wa nguo nchini Rashid Said maarufu kama Chid Mapenzi. Mahusiano yao yalidumu kwa takribani miezi mitatu kabla ya kuamua kufunga ndoa na kuwa na mke na mume.

 

Mapenzi yao yalitawaliwa na furaha na amani mwanzoni na kwa kiasi kikubwa yaliwavutia watu wengi. Chid Mapenzi kipindi hiko alikuwa anamiliki maduka ya nguo katika maeneo tofauti tofauti katika jiji la Dar es Salaam, huku Shamsa Ford yeye akijishughulisa na kazi yake ya uigizaji.

 

Kwa kuwa Chid Mapenzi shughuli zake nyingi zilikuwa zipo nchini China ilimbidi awe arudi nchini China na kumuacha mke wake nyumbani Tanzania akisimamia biashara za mume wake. Chid Mapenzi pia alilazimika kusafiri mara kwa mara kurudi nchini kuja kuisalimia familia yake.

 

Kama wasemavyo waswahili kuwa vikombe kwenye sinia havikosi kugongana ndivyo ilivyotokea kwa ndoa hii ya Chid Mapenzi na Shamsa Ford kwani kuanzia mwaka 2017 tetesi zikaanza kuwa hawapo katika maelewano mazuri. Maneno yalikuwa mengi mpaka kwenye mitandao ya kijamii kurasa za udaku zilikuwa zikiripoti taarifa hizo kila siku.

 

Chanzo cha sintofahamu hiyo ilitajwa kuwa ni kukosa mtoto katika ndoa yao. Chid Mapenzi na mke wake mara nyingi walikanusha taarifa hizo wakisema kuwa kila mtu ana mipango yake katika ndoa yoyote ile kwani wengine hupanga kupata watoto hata kuanzia miaka 5 hivyo kwanini wawashangae wao ambao wana mwaka mmoja tu kwenye ndoa.

 

Maisha yalisonga mbele huku amani, furaha na hata migogoro ikitokea kama ilivyokuwa hulka ya wanadamu. Mwaka 2018 ndoa ya Chid Mapenzi na Shamsa ilionekana kukalia kuti kavu baada ya kusambaa habari kuwa wawili hao wapo kwenye mgogoro mkubwa na wengine wakitaja chanzo kuwa ni kushuka kipato kwa Chid Mapenzi hivyo Shamsa kashindwa kuvumilia kabisa.

 

Wengine walienda mbali zaidi wakisema chanzo cha ugomvi wao ni mtoto wa Shamsa Ford aitwaye Terry. Mtoto huyo alimpata na mwanaume mwingine kabla ya ndoa na Chid Mapenzi.

 

Ikasemwa kuwa Chid Mapenzi hakuwa anaonysha mapenzi kwa mtoto huyo jambo ambalo lilikuwa likimuumiza Shamsa Ford. Baadae Shamsa Ford alikuja kukiri kuwa Chid Mapenzi aliwahi kumdai dolla 100 alizomuazima ili kwenda kulipa ada ya mtoto wake shule anasema jambo hilo lilimchukiza sana.

 

Mwaka 2019 baada ya kuzungumzwa mengi ndoa ya Chid Mapenzi na Shamsa Ford ikavunjka rasmi na kila mtu kujua mambo yake ambapo Shamsa Ford aliendelea na biashara yake ya kuuza madira na vijora katika duka lake lililopo mitaa ya Mwananyamala na Chid Mapenzi naye akaendelea na mambo yake ambapo anaendelea na uuzaji wa nguo.

 

Baada ya ndoa yao kuvunjika na siku nyingi kupita hasira baina yao zikaisha na kuanza ukurasa mpya wa maisha ambapo wameamua kuwa kama kaka na dada na hapo kuzika tofauti zao.

Leave A Reply