The House of Favourite Newspapers

Shehe mkuu atoa neno

0

AlhadiMussaSalumNa Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO

DAR ES SALAAM: Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa ametoa neno kwa wananchi wote na hasa Waislamu, akiwataka kuishi kwa maadili na matendo mema, wakati huu wakiwa wameanza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Shehe Alhad alisema kufunga Ramadhan ni lazima kwa kila Muislamu, hivyo tabia ya baadhi yao kutoa visingizio vya kusumbuliwa na magonjwa kama vidonda vya tumbo, moyo na kadhalika inapaswa kuachwa mara moja kwani wanamchukiza Mwenyezi Mungu.

Aidha, alisema mwezi huu ni semina kwa Waislamu hivyo wanatakiwa kuutumia kwa kuomba amani ya nchi pamoja na kumwombea Rais John Pombe Magufuli ambaye amejitoa kwa ajili ya kuwatumikia ili Mungu azidi kumlinda na kumwepusha na mabaya.

“Waislamu watumie mwezi huu kuombea amani ya Tanzania ili mauaji yanayoendelea yaishe, pia kumuombea Rais Magufuli aweze kuendelea na kazi nzuri anayoifanya na awe na afya njema kwani amejitoa kwa moyo wote kuwatumikia Watanzania,” alisema Shehe Alhad.

Kwa upande mwingine, aliwataka wasanii wa fani mbalimbali kuuheshimu mwezi huu mtukufu kwa kujisitiri na kuacha kuvaa nguo za ajabu na kufanya mambo maovu, hasa starehe na unywaji pombe, kitu alichosema kinapaswa kuendelea kufanywa hata baada ya mwezi huu kumalizika.

Leave A Reply