The House of Favourite Newspapers

Shehe Ponda amkumbusha Magufuli mgogoro wa Zanzibar

1

3.Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Issa Ponda akizungumza na wanahabari.

2.Wanahabari wakiendelea kupata ufafanuzi kutoka kwake.

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Issa Ponda amemkumbusha Rais Dk. John Pombe Magufuli kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar.

Ametoa kauli hiyo leo katika Msikiti wa Kichangani jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari juu ya namna Dk.Magufuli anavyoweza kutatua mgogoro huo ili kuzuia machafuko kwani kuna viashiria vya machafuko kipindi hiki.

Ponda alisema Rais Magufuli anao wajibu wa kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati akihutubia Bunge kuwa ndio suluhisho la mgogoro huo wa kisiasa pasipo kusababisha Zanzibar kuingia katika dhiki na uhasama uliopitiliza.

Aidha, alisema msajili wa vyama vya siasa nchini pia anaweza kuingilia kati mgogoro huo kwani anayo mamlaka ya kuwakutanisha viongozi wa kisiasa wa pande mbili za CCM na Cuf kwa kukaa na kutafuta suluhu ya mzozo huo.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

1 Comment
  1. winnie s says

    Ponda kwa kweli in sikio la kufa halisikii Dawa.Ivi akihubili dini pekee waumini wake hawata mwelewa.Ponda nikuombe jambo moja bado miaka mi NNE subili ugombee nafasi yoyote ya juu.Unamkumbusha JPM wetu .sasa wewe kama nani. Ponda tuache watanzania tu lale na laha zetu.

Leave A Reply