The House of Favourite Newspapers

Shehena ya Mionzi ya Nyuklia Haijafika Dar

0

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imesema shehena iliyokuwa na viasili vya mionzi ya nyuklia iliyokuwa kwenye meli MV SEAGO PIRAEUS VOY 174S ikisafirishwa (Transshipment) kuja Tanzania kupitia Bandari ya Mombasa haikufika nchini.

Imesema Mamlaka ya Udhibiti wa Mionzi ya Nyuklia Nchini Kenya (Kenya Nuclear Regulatory Authority-KNRA) ili ilichukua hatua stahiki na shehena kuamriwa kurejeshwa ilikotoka.

Kwa taarifa za Jumatano Tarehe 22 Disemba 2021, saa sita na nusu usiku 00:30 (00:30 LT(UTC+4)) meli hii ilikuwa imetia nanga Nchini Oman katika bandari ya Salalah.

“TAEC inapenda kuwatoa hofu watanzania wote kuhusiana na taarifa ya tukio hilo kwani shehena hiyo haikufika nchini. Hata hivyo, Serikali iko macho na imejipanga vyema katika udhibiti wa uingizaji vyanzo vyote vya mionzi kupitia Bandari na sehemu zote za mipaka nchini,” imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Leave A Reply