The House of Favourite Newspapers

Sheikh Ponda Afunguka Sakata la Mali za BAKWATA Kuishauri Serikali

0
Sheikh Ponda Issa Ponda.

KATIBU wa Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema wanajipanga kuishauri Serikali namna bora ya kupata suluhu dhidi ya mali za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ambazo ziko katika uchunguzi.

Sheikh Ponda ametoa kauli hiyo leo tarehe 2 Mei 2023, ikiwa ni siku chache tangu baadhi ya wajumbe wa tume iliyoundwa kuchunguza mali na madeni ya BAKWATA, kujiuzulu kwa madai kwamba walikabiliwa na ugumu katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Kwa sasa tunajipanga kuboresha maeneo ambayo tunapanga kuzungumzia ikiwemo aina ya Mali hizo, nani muasisi na mmiliki halali, Hali ya mali hizo sasa ikoje na ushauri Wetu kwa Serikali na BAKWATA. Tunataraji baada ya kukamilisha maboresho tutaeleza kwa umma tunachokishauri,” amesema Sheikh Ponda.

Wajumbe wanne tume hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Sheikh Issa Issa, mnamo tarehe 30 Aprili 2023,waliandika barua ya kujiuzulu katika majukumu hayo kwa Maelezo kwamba ni kutokana na ugumu katika kutekeleza majukumu Yao.

Wajumbe wengine waliojiuzulu ni, Mohamed Nyegi, Daud Nasib, Idi Kamazima na Omari Igge.

Mnamo Februari mwaka huu, Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir, aliunda Tume ya Maboresho ya BAKWATA, ambayo aliipa majukumu mbalimbali ikiwemo kuchunguza mali na madeni za baraza Hilo kwa ajili ya kuangalia namna bora ya kulipa madeni na kuzitunza Mali hizo.

BUNGE ZIMA LACHEKA🤣 MBUNGE MUSUKUMA AKICHANGIA kwa KINGEREZA – “YOU NEED TO BE VERY IGNORANT”…

Leave A Reply