The House of Favourite Newspapers

Spika Tulia Aomba Jimbo lake la Mbeya Mjini Ligawanywe

0

 

 

Spika wa Bunge, Tulia Ackson  ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.

Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.

Katika swali lake Mwakagenda ameuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.

“Kama Serikali tunatambua lakini nikuhakikishie, Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni Spika wetu Tulia ameshawasilisha suala hili na lipo mezani kwahiyo muda utakapofika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itatizama pia Jimbo la Mbeya Mjini.” Amesema Naibu Waziri Ummy akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda.

BUNGE ZIMA LACHEKA MBUNGE MUSUKUMA AKICHANGIA kwa KINGEREZA – “YOU NEED TO BE VERY IGNORANT”…

Leave A Reply