The House of Favourite Newspapers

Shigongo Aendelea Kuchanja Mbuga Buchosa

0

MGOMBEA ubunge Jimbo la Buchosa, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo, ameendelea na shughuli zake za kampeni kwa wakazi wa jimbo hilo, ambapo leo amefanikiwa kuanza kampeni zake kwa kuzungumza na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kata ya Kafunzo.

 

Kampeni za Shigongo leo zimefanyika katika maeneo matatu tofauti, ambapo kikao cha kwanza kilianzia katika shule ya Sekondari Kafunzo, kisha  kijiji cha Bilulumo, Luholongoma na kisha kumalizia katika uwanja wa mpira wa miguu wa Kafunzo.

 

Akizungumza kwenye mikutano hiyo, Shigongo ameahidi kujenga daraja la Chintu lililopo kwenye kijiji cha Luholongoma, mbali na hivyo pia ameahidi kununua greda lake mwenyewe kwa ajili ya kuhakikisha anakarabati barabara zote za jimbo hilo kila zinapoharibika.

 

Mbali na hivyo,  amesema atahakikisha anaboresha suala la upatikanaji wa miundombinu ya umeme kwenye vijiji vyote vilivyosalia kama kanuni ya CCM ilivyotamka.

 

Pia amewataka wananchi wa jimbo hilo kuachana na ubaguzi wa makabila na dini, kwani kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kuwagawa wananchi.

 

Ahadi kama hizo alizitoa jana alipokuwa kwenye mikutano yake iliyofanyika kwenye kijiji cha Chema alipokuwa akimnadi diwani wa kata ya Bupandwamhela, Masumbuko Francis Bupamba, na katika kijiji cha Katwe ambapo aliahidi kuwasaidia na wananchi wa kata hizo kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya katika shule na zahanati ya Katwe ya kata hiyo.

 

Mkutano wake wa jana (Ijumaa) ulimalizikia katika kijiji cha Kahunda ambapo aliahidi pia kuboresha miuondombinu ya barabara na vitendea-kazi vya uvuvi katika Ziwa Victoria lililopo kwenye mwambao wa kijiji hicho.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave A Reply