Shigongo Akagua Ujenzi wa Shule Mpya na Zahanati Buchosa

Mbunge wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kahunda kata ya Katwe alipofanya ziara kijijini hapo.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo amefanya mikutano miwili ya hadhara katika Kijiji cha Kahunda na Katwe na kuzingumza na wananchi wa vijiji hivyo akieleza Mambo mbalimbali aliyoyafanya katika kipindi kifupi tangu alivyochanguliwa mwishoni mwa mwaka jana.

Shigongo ameeleza kuwa baadhi ya mambo ambayo amekwishafanya ndani ya siku 160 za uongozi wake ni pamoja na ujenzi wa barabara, ujenzi wa madarasa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari, Zahanati, uchimbaji wa visima virefu vya maji pamoja na mambo mengine mengi.

Shigongo pia alitoa fursa kwa wananchi wa vijiji hivyo kueleza kero na changamoto zinazowakabili kwenye vijiji vyao ambapo ametatua papo kwa papo kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi kwenye mikutano hiyo.

Aidha, Shigongo alikichukua mawazo na ushauri kutoka kwa wananchi wake ili aweze kuzifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuziwasilisha katika Mbunge la Jumuhuri ya Muungano wa Tanzania ziweze kujadili kwa maslahi mapana ya wananchi wa Buchosa na Taifa kwa ujumla.

 

Shigongo amefanya ziara na kukagua ujenzi wa Zahanati ya Katwe ambayo ilijengwa kwa nguvu za wananchi huku akitoa Tsh million 10 kutoka mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kuezeka zahati hiyo.

 

 

 

 

Aidha, Mhe. Eric Shigongo akipata maelekezo ya ujenzi wa shule mpya ya msingi Milimani katika kata ya Katwe pamoja na jengo la zahati zilizojengwa kwa nguvu za wananchi.

Shigongo amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Kahunda kwa kuamua kujitolea kujenga majengo hayo ili kusaidia watoto wao pamoja na kupunguza idadi kubwa ya wanafunzi katika shule ya msingi Kahunda na kusogeza huduma ya afya karibu.

Shigongo ameahidi kuwasaidia kuongeza madarasa mengine katika shule hiyo mpya ya Mlimani.

 

Mhe. Eric Shigongo amefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katika kata ya Katwe ambapo ametembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili na matundu saba ya vyoo katika shule ya msingi Kahunda vilivyo gharimu kiasi cha shilingi million 47 fedha zilizotolewa na serikali.

 

 

 Tecno


Toa comment