The House of Favourite Newspapers

Shigongo Atikisa Buchosa: Lami Inapita Hapa – Video

0

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, ameendelea na kampeni za kunadi sera zake na kuomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo ili waweze kumpa ridhaa ya kuwa mbunge wao kwa miaka mitano ijayo.

 

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Irenza, amesema kuwa haoni kama kuna chama bora nchini Tanzania kama CCM kwani hata demokrasia yake ni kubwa na viongozi wamekuwa wakiachiana madaraka kwa amani kuanzia enzi za Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa, Jakaya Kikwete na Dkt. John Magufuli.

 

Aidha, Shigongo amewaahidi wananchi hao kuwa iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wao basi atahakikisha anawaletea maendeleo thabiti ambayo hawajawahi kuyapata tangu enzi za Uhuru. 

 

“Nitafanya kazi kubwa na nyinyi kwa miaka mitano, na lami mpya itapita hapa, tangu uhuru hapajawahi kuwa na lami Buchosa, mwezi Desemba inaanza kujengwa lami mpya na mimi ndiyo niliyeiomba kwa Mheshimiwa Rais, naomba mniamini, mnipe kura zenu Oktoba 28,” amesema Shigongo.

 

Leave A Reply