The House of Favourite Newspapers

Shigongo Awatia Moyo Wanafunzi Vyuo Vikuu Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group na Mhamasishaji Maarufu Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar es Salaam.

MKURUGENZI Mtendaji wa Makampuni ya Global Group na Mhamasishaji Maarufu Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo amewaasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo  vyuo vikuu vya jijini Dar es Salaam, kutokukata tamaa katika kutafuta mafanikio katika maisha yao.

Sehemu ya umati wa wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo.

Akizungumza katika kwenye Kongamano la Chuo Life Time 2018 lililoandaliwa na Taasisi ya Chuo Life Tanzania na kuwakutanisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa vyuo vikuu vya Dar es Salaam katika ukumbiwa wa Yombo 4 uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Saalam, Shigongo amewataka vijana hao kujitoa kwa nguvu zao zote ili kufanikiwa na kutimiza ndoto za maisha yao.

Shigongo amesema kuwa changamoto katika maisha ndiyo iwe suluhisho la mafanikio yao, hivyo watumie nafasi hizo kama fursa ya kutatua changamoto na mwisho wake ni mafanikio.

Shigongo akizungumza na wanafunzi hao.

Amerudia kauli yake ya kila siku ya kwamba kila mmoja aliyehudhuria katika kongamano hilo hajapoteza muda wake bali Mungu ameona ni siku pekee kwake kuondoka na matunda ya mafanikio na hivyo wanafunzi hao tayari wamekuwa matunda ya kesho katika familia zao.

Sehemu ya umati wa wanachuo waliohudhuria kongamano hilo.

Amewataka wanafunzi hao kutokuangalia mataifa mengine yaliyofanikiwa hivyo wao ndiyo wawe wa kwanza kuipenda nchi yao na kuiletea maendeleo na hapo ndipo wataweza kulinufaisha taifa lao.

Mmoja wa washiriki wa Kongamano hilo.

Akitolea mfano wa kutokukata tamaa kwa vijana, Shigongo amesema kuna binti aitwaye Asia Mustafa mkazi wa Dar es Salaam, yeye alipatwa na tatizo la figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi akiwa mdogo, wazazi wake walisumbuka mahospitalini hadi kumfikisha India ambako alifanyiwa upasuaji, akaondolewa figo zote na kupandikizwa figo moja ya mtu mwingine.

Mshindi wa Taji la Miss Tanzania 2016, Dyana ambaye ni mwanafunzi wa IFM naye akiwatia moyo wanafunzi wa mwaka wa kwanza.

Lakini baadaye figo hiyo nayo ilishindwa kufanya kazi hivyo mpaka sasa hana figo mwaka wa 12 sasa, anaishi kwa kufanyiwa dialysis (kuondoa maji yaliyozidi na sumu mwilini) katika Hospitali ya Muhimbili kila wiki, lakini mpaka sasa hajakata tamaa na ameandika kitabu chake ambacho kimeshakamilika kikielezea maisha yake.

Benjamin Fernandes akionyesha diary yenye orodha ya kazi zote anazofanya kila siku.

Mbali na Shigongo, wengine waliohudhuria na kupata fursa ya kuzungumza na wanafunzi hao ni Mtaalam wa Mambo ya Saikolojia na Mahusiano, Dkt. Chris Mauki, Mshindi wa Miss Tanzania 2016, Diana Edward, Benjamin Fernandes na wengine.

Chris Mauki akizungumza na wanafunzi hao.

Lengo la CHUO LIFE TIME 2018 ilikuwa ni kumjengea kijana uwezo kujitambua na kutambua Thamani aliyoibeba kwenye maisha yake katika safari ya mafanikio, kutambua fursa na Changamoto za maisha ya chuo na kuzitumia katika kufanikisha malengo yake.

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.