The House of Favourite Newspapers

Shigongo Azindua Kampeni ya ‘Buchosa Mpya’ – Video

0

MBUNGE wa Buchosa, Eric Shigongo leo Januari 26, 2021, amezindua rasmi kampeni ya Buchosa Mpya, Peleka Mtoto Shule ambao umefanyika katika kata ya Nyanzenda.

 

Katika uzinduzi huo amepokelewa kwa shangwe na wanafunzi wa shule hiyo ambapo jumla ya wanafunzi 200 wamepewa sare za shule na madaftari kwa watoto wanaotoka familia zisizojiweza, madaftari 6,014 kwa wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule za kata tisa kati ya 21 za jimbo hilo zilizofikiwa mpaka sasa lengo likiwa ni kufikia wanafunzi zaidi ya 500 kutoka familia zisizojiweza na wanafunzi zaidi ya 9,000 wa darasa la kwanza.

 

 

Akingumza kwenye uzinduzi huo, Shigongo amesema ameamua kusaidia Watoto kielimu ili kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shule na kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli kutoa elimu bila malipo huku akiwasisitiza Watanzania kuwahimiza watoto kusoma kwa elimu.

 

 

“Wazazi tunawajibu mkubwa wa kuhimiza na kuwasimamia watoto wetu kusoma kwani elimu ni njia pekee ya kuondokana na umasikini katika familia na jamii yetu na kufikia maendeleo kwenye nchi yetu kampeni hii iwe chachu ya kuinua elimu katika Jimbo letu la Buchosa na Tanzania kwa ujimla,” amesema Shigongo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply