The House of Favourite Newspapers

Shigongo: Bila Maarifa Hakuna Mafanikio

Shigongo (1)Mchungaji Muabuzi akitoa neno kwa waumini (hawapo pichani).Shigongo (5)Mgeni rasmi, Eric Shigongo akitoa neno wakati wa uzinduzi wa kitabu kipya cha Njia ya Mafanikio cha Mchungaji Muabuzi.
Shigongo (3)
…wakiwa katika maombi.Shigongo (7)…kwa pamoja wakionesha kitabu hicho.
Shigongo (6)
Shigongo akionesha kitabu kipya cha Njia ya Mafanikio.

Na Mwandishi Wetu

MHAMASISHAJI wa kimataifa wa watu kujikomboa na umaskini, Eric Shigongo, amesema bila kuwa na taarifa au maarifa stahiki, ni vigumu kwa mtu yeyote kufikia mafanio yake.

Shigongo aliyasema hayo jana Jumapili, ndani ya Kanisa la Hossana Life Mission, lililopo Ubungo jijini Dar, alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu cha Njia ya Mafanikio, kilichoandikwa na Mchungaji Muabuzi, kinachoelezea siri mbalimbali za mafanikio na jinsi ya kuyapata mafanikio hayo.

Awali, kabla ya kumkaribisha Shigongo, Mchungaji Muabuzi alisema kanuni alizoziandika katika kitabu hicho, zikitumiwa na mtu kwa vitendo, hakika ni lazima maisha yake yabadilike na ndoto kutimia.

“Mungu ameniongoza vyema mno katika kukiandaa kitabu hiki, endapo kama mtu atakisoma na kuzitumia vyema kanuni hizi, hakika lazima maisha yake yabadilike na furaha itimie,” alisema Muabuzi.

“Bila maarifa, hakuna mafanikio katika maisha, zipo kanuni ambazo ni lazima mtu azifuate ili kufikia malengo ya maisha yake, miongoni mwa kanuni hizo ni kutafuta maarifa, na maarifa yanapatikana katika maandishi, kwa maana ya vitabu, bila maarifa si rahisi mtu kufanikiwa,” alisema Shigongo.

Comments are closed.