The House of Favourite Newspapers

Shigongo Ashuhudia Kambi ya Wavuvi Ilivyotekea, Mmoja Afariki, Mamia Wapoteza Makazi

0

 

 

Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe Eric Shigongo, amewatembelea wahanga wa moto kambi ya uvuvi ya Migongo iliyoko katika Kata ya Maisome Jimbo la Buchosa na kujionea mwenyewe hali halisi ya janga hilo.

 

 

Katika janga hilo lililotokea Jumanne ya Mchi 9, mwaka huu 2021, kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Mussa Edward alipoteza Maisha wakati akitibiwa kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kulipukiwa na mafuta ya petrol wakati anakoa mali zake.

 

 

Mbali na kifo hicho, baadhi ya wakazi wengine na wafanyabiashara wa maeneo hayo waliunguliwa na nyumba zao huku mali zao zikiharibiwa vibaya na moto huo ambapo watu 100 wamepoteza makazi yao baada ya nyumba zao kuteketea kwa moto.

 

Akizungumza na wananchi wa Migongo, Mhe. Shigongo viongozi wa Halmashauri hiyo kufanya tathimini ili waweze kuwasaidia watu waliotoza mali zao na makazi yao kutokana na moto huo.

 

 

Aidha, Mhe. Shigongo amemtaka Mwenyekiti wa kambi la uvuvi migogo Masau , Malegesi atumie uwazi wakati misaada hiyo itakapofika ili kuondoa mkanganyiko unaweza kujitokeza.

 

 

Diwani wa kata ya Maisome Dauson Miyaga amemshukuru mbunge, kufika na kuwaona watu waliopoteza mali zao kutokana na ajili ya moto.

 

Leave A Reply