The House of Favourite Newspapers

Shigongo: Mniamini Tuibadilishe Buchosa

0

MGOMBEA ubunge Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, amewasisitiza kwamba wamwamini na kumpa kura za kuwa mbunge wakijua kabisa ataleta mabadiliko makubwa katika maisha ya wananchi wa  jimbohilo.

 

Akizungumza katika Kijiji cha Luhama, Kata ya Bangwe, wakati wa mkutano wake wa kampeni  zinazoendelea, amewaahidi kwamba atakuwa mtumwa kwao ili kuwatumikia huku akiwasisitiza kujiandaa kufanya kazi kwa bidii kutokana na yeye kuamini katika kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya maendeleo.

“Ndugu zangu mimi nitakuwa mtumwa kwenu katika kuwaletea maendeleo, hivyo ninachowaomba mjiandae kufanya kazi kwa bidii kwani kiongozi wenu anaamini mafanikio yanakuja kwa kujitoa na kufanya kazi kwa bidii.  Tukishirikiana kwa pamoja mabadiliko ya Buchosa yanawezekana na hamtaamini. Ndugu zangu, ninawaomba mniamini tuibadilishe Buchosa yetu,” amesema.

 

Leave A Reply