The House of Favourite Newspapers

Shime: Tutawafunga Nyingi Burundi Tena

0

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wasichana wa U17, Kilimanjaro Queens, Bakari Shime amesema kuwa watawafunga Burundi kwa mabao mengi katika mchezo wa marudiano utakaochezwa kesho Jumamosi katika Jiji la Bujumbura, Burundi.

 

Tanzania waliibuka kwa ushindi wa mabao 5-1, katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar, wiki moja iliyopita, ikiwa ni mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia, itakayofanyika nchini India, kati ya mwezi Juni au Julai.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Shime alisema wanakwenda kushinda kwa idadi kubwa ya mabao kama ilivyokuwa katika mchezo wa awali, kwani walifanya marekebisho katika maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa na upungufu, huku akiongeza kuwa Burundi hawana uwezo wa kupindua matokeo hata kama watakuwa wanacheza mbele ya mashabiki wao.

“Tunakwenda Burundi kwa lengo la kuvuna ushindi mwingine mkubwa, tuliwafunga 5-1 hapa nyumbani, tunaenda kuwafunga nyingine nyingi wakiwa kwao, kwa sababu watakuwa wanacheza kwa presha ya kutaka kupindua matokeo, kitu ambacho kwao ni kugumu kufanikiwa, lakini sisi tumerekebisha baadhi ya upungufu uliojitokeza katika mchezo wa kwanza,” alisema Shime.

 

Kili Queens waliondoka jana mchana kuelekea Burundi, tayari kwa mchezo huo ambapo wakifanikiwa kushinda watakuwa na mechi nyingine nne, ambazo pia wanatakiwa kushinda ili wafuzu kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

Leave A Reply