The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba… droo ya 3 kufanyika leo

0

SHINDA NYUMBA (10)

Mshindi wa droo ya pili ya Shinda Nyumba alivyokabidhiwa pikipiki.

Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kufanyika kwa kishindo kwa droo ya kwanza na ya pili, sasa droo nyingine ambayo itakuwa ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na kampuni inayochapisha Magazeti ya Uwazi, Amani, Championi, Ijumaa, Risasi na Ijumaa wikienda, Global Publishers itafanyika leo, Machi 30 katika Viwanja vya Manzese-Bakhresa jijini Dar.
SHINDA NYUMBA (1)Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda aliwaomba wasomaji wa magazeti hayo kujitokeza kwa wingi na kushuhudia droo hiyo ikichezeshwa kwani wanaweza kuwa washindi.

8.Kuponi za Bahati nasibu ya Shinda Nyumba zikiwekwa katika ndoo maalum ya Shinda Nyumba.

“Kila mfuatiliaji wa magazeti ya Global Publishers anatambua zawadi zinazotolewa kila droo ikifanyika. Droo ya kwanza tulimpata mshindi wa zawadi kubwa ya TV Flat Screen pamoja na King’amuzi cha Ting, Happyness Haule na waliobakia wote walipata zawadi kabambe kama vile seti ya vyombo vya ndani, simu za kisasa (smart phone), ving’amuzi vya Ting na nyingine nyingi.

7.Wakazi wa maeneo ya Goba jijini Dar wakihamasikia kujaza kuponi zao na kushiriki droo ya shinda nyumba.

“Katika droo ya pili pia tulishuhudia kwa mshindi kutoka Kibaha, Pwani ambaye ni Lucy Swai aliyejinyakulia zawadi ya Pikipiki ya Skymark huku zawadi nyingine kabambe zikitolewa. Mshindi wa leo anaweza kuwa ni wewe, hivyo jaza kuponi kisha tukutane, Manzese kwa droo ya tatu,” alisema Mkanda.

3.Yohana Mkanda (katikati) akijaribu kuwapa maelekezo ya jinsi namana msomaji wa magazeti ya Global anavyoweza kujishindia nyumba.

Katika droo kubwa, mshindi atazawadia nyumba ya kisasa iliyopo Salasala-Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ikiwa na samani za ndani. Katika shindano hili watu walio chini ya umri wa miaka 18, ndugu wa wafanyakazi wa Global Publishers hawaruhusiwi kushiriki.

Leave A Reply