The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba… Makonda Ndiye Mwenye Siri

0

Shinda Nyumba na Global (6)     Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

KAMA wewe ni muumini wa kitu kinaitwa dili, basi ili uipate nyumba ambayo ndiyo zawadi kubwa kabisa itakayotolewa katika kilele cha Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba ya Global Publishers, fanya dili na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mimi huwaga siamini katika dili, maana mara nyingi huwa siyo kwa njia halali. Lakini watu tunatofautiana bwana, maana kila mtu na imani yake, wengine maisha yao yote ni ya dili, ndiyo maana wanadiriki hata kusema kuwa hakuna ukweli katika utoaji wa nyumba hii, bali kilichopo ni dili tu, eti watapeana wenyewe kwa wenyewe.

Nyumba-7Basi kama wewe unaamini katika hilo, ndiyo maana ninakuambia wahi pale Ilala Boma, zilipo ofisi za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ukapange naye dili ili uibuke na nyumba hii yenye thamani ya mamilioni ya shilingi, iliyopo Salasala nje kidogo ya jiji ikiwa na samani za kisasa ndani yake.

Hii ni kwa sababu Makonda, mmoja wa viongozi vijana ambao Rais John Magufuli anajivunia, ndiye atakayefungwa kitambaa usoni, kisha atachanganya kuponi na baadaye ataichagua moja ambayo ndiyo itakuwa ya mshindi wa shindano hili lililodumu kwa miezi sita sasa.

Nyumba-3Tukio hili litafanyika Alhamisi hii katika Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na maofisa kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, ambao ndiyo wasimamizi wa michezo yote ya kubahatisha nchini.

Nyumba-4Niendelee kuwasihi wasomaji wote wa magazeti ya Global Publishers, ambayo ni Uwazi, Ijumaa, Championi, Risasi, Amani na Ijumaa Wikienda, wahisha kuponi yako sasa, kwa sababu muda uliobaki ni mdogo. Nenda kwa wakala wa magazeti hayo popote Tanzania, mpatie kuponi zako naye atajua jinsi gani ataziwasilisha kwetu haraka, lakini kwa wale walio Dar es Salaam, nenda mwenyewe zilipo ofisi za magazeti hayo, Bamaga, Mwenge.

Nyumba-2Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, maandalizi yote kwa ajili ya tukio hilo kubwa yamekamilika na kinachosubiriwa ni siku tu ili msomaji wake mmoja aingie katika orodha ya wamiliki wa mijengo ya thamani kubwa katika jiji.

Nyumba-5Kama ambavyo imekuwa ikielezwa mara kwa mara ni kuwa mjengo huo wa kileo, wenye samani za kisasa, umekamilika na unamsubiri mshindi ambaye kwa vyovyote, kama siyo wewe, basi atakuwa ni msomaji mwingine aliyeshiriki pamoja nasi tangu mwanzo.

Licha ya zawadi hiyo kubwa, pia siku hiyo kutakuwepo na zawadi nyingine nyingi ndogondogo zitakazotolewa, kama vile kofia, fulana na kadhalika, ilimradi tu Global Publishers haitaki kumuacha msomaji wake arudi mtupu nyumbani.

Leave A Reply