The House of Favourite Newspapers

Shoga; lazima kubadili eneo la tukio

0

Couple-in-BedNi Jumanne tena, namshukuru sana Mungu kwa ajili ya siku hii njema kwangu, naamini na kwako pia.

Leo bado naendelea na mazungumzo ya wanawake wenzangu na nitazungumzia tabia inayochosha kwenye eneo la kujiachia na wanaume zetu.

Kumekuwa na kawaida kwa baadhi ya wanawake, tena naweza kusema sehemu kubwa ya wanawake, wanachojua wao ni kwamba, kutimiza tendo ni lazima iwe kwenye sita kwa sita tu!

Naamini wapo wanawake wenzangu ambao wakiambiwa na waume zao kubadili mandhari, wanakuja juu wakiamini kwamba, wanaume hao watakuwa wamechanganyikiwa au wameanza tabia mbaya.

Hilo si jambo la kweli jamani wanawake wenzangu. Hata nyie mkifikiria sana mtagundua kwamba, kunachosha. Yaani kila siku mcheze kwenye uwanja wa taifa tu, lazima itafika mahali utaona unakinai kwa vile kila siku ni uwanja huohuo tu.

Ni jambo jema ukakaa na mwenza wako, mkakubaliana kwamba, siku nyingine muhame uwanja, mnaweza kuhamia uwanja mwingine hata ulio kando ya mji.

Hii husaidia kukutana na mazingira mageni na pia kitendo cha kukutana na mazingira mageni husaidia kunogesha chachu ya mahaba yenyewe.

Unajua mambo haya ya kutimiza tendo ni kama kula chakula tu. Leo ukipewa ugali, maharage, kesho ugali maharage lazima utafika mahali utaanza kushindwa kula.

Ndiyo mahaba nayo, kila siku uwanja wa taifa, kila siku hapohapo tu. Lazima itafika mahali utamshangaa mwenzako anapitisha wiki bila kukuingiza uwanjani ukiuliza sababu, atakwambia amechoka, kazi nyingi.

Huo ni uongo, hakuna cha kuchoka na kazi hapo, ila amechoshwa na matumizi ya uwanja mmoja kila siku. Anataka uwanja mpya.

Wapo wenzetu ni wabunifu sana, wao kila siku wanatafuta uwanja mpya. Leo anachezea uwanja wa chumbani, kesho anakwenda uwanja wa sebuleni, siku nyingine hadi anafika uwanja wa sehemu ya kuogea.

Ubunifu huu umekuwa ukisaidia sana kuboresha mapenzi sambamba na kumfanya mwanaume awe anawahi kurudi nyumbani kwa vile anamisi viwanja.

Tabia ya kutumia uwanja mmoja ni ya kizamani sana, kule vijijini ambapo pia, wanaume wa wakati huo walikuwa waaminifu sana kwa wake zao. Kwa miaka ya siku hizi, wanaume wetu wa mijini hawa, ukiwafanyia hivyo, uwanja ni huohuo tu, hawakawii kuchepuka.

Ndiyo maana utaona mume wa mtu anakuwa na nyumba ndogo hata tano, kwa sababu ya kutafuta mazingira mageni kila kukicha.

Na wanawake wa mijini wa siku hizi, akishajua huyu ni mume wa mtu, wee! Anampoteza kabisa kuiwaza familia yake. Leo atampeleka Bagamoyo, kesho katikati ya jiji, keshokutwa Kigamboni, wewe umebaki nyumbani tu unasubiri mume aje muingie uwanja wa taifa!

Lazima uwe mbunifu shoga, kila siku angalia kitu kipya ni kipi! Uwanja mpya ni upi! Hii unajumuisha hadi kwenye kupaka mafuta, losheni na mambo mengine.

Wengine kila wakipanda kulala wanapaka mafuta ya nazi. Wakiamka mafuta ya nazi, wakienda mtoko, mafuta ya nazi. Jamani, huyo mume si atajua wewe ni yuleyule wa miaka ile! Badilikeni wanawake wenzangu.

Wanaume si watu wa kuwakaririsha jambo moja kila siku, huwa wanachoka haraka sana. Mwangalie sana mumeo jambo gani linamchosha, wengine wameumbwa wazito wa kusema la moyoni.

Tuonane wiki ijayo.

Leave A Reply