The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Yatikisa Kiwagwa, Nyumba Mpya Kutolewa Sept. 27

0
Ndekeleni William katiakti wakati wa droo.

ZIKIWA zimebaki takribani wiki mbili ili kuchezeshwa kwa droo kubwa katika Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili zikikatika kwa kasi, macho yote ya wasomaji wa magazeti ya Global Publishers yameelekezwa kwenye zawadi hiyo kubwa ya nyumba.

 

 

Leo Septemba 11, timu nzima ya Shinda Nyumba iliibukia maeneo ya Kiwangwa Bagamoyo Pwani na kugawa zawadi lukuki kwa wasomaji wa Magazeti yanayochapishwa na Global Publishers ya Uwazi, Championi, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Ijumaa baada ya kuchezesha bahati nasbu ndogo eneo hilo huku wasomaji kadhaa wakiibuka washindi na kukabidhiwa zawadi hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Kiwagwa wameahidi kuendelea kushiriki zaidi ili wajihakikishie ushindi wa nyumba hiyo mpya.

 

 

“Yaani kama mimi, akili yangu ni juu ya nyumba tu, nimejitahidi nikakata kuponi nyingi na hata sasa ninaendelea kukata kwa kila nakala inayotoka, nadhani hii ni nafasi yangu kuibuka mshindi,” alisema Ndekeleni William.

 

Mrisho Kimosa akijaza kuponi.

Naye Maneno Mohammed, amesema hakuna mtu aliyekata kuponi za bahati nasibu ya Shinda Nyumba ambaye hafikirii kuhusu zawadi hiyo kubwa ambayo ina thamani ya mamilioni ya shilingi. “Ninachoweza kukuambia ni kwamba hakuna mtu mwenye kuponi ambaye hafikirii kuhusu hiyo nyumba.

 

Hivi ni nani asiwazie nyumba ya mamilioni ya shilingi kuipata kwa shilingi mia tano tu? Kwa kweli mimi binafsi naona hili zoezi linachelewa, bora huu mchezo uishe tu tuwaze vitu vingine maana akili yote inatembea nyumba, nyumba,” alisema Victoria Kolombani.

 

Kuponi zikichanganywa kwenye ndoo kupata mshindi wa zawadi ndogo.

Nelly Mwangosi, mama wa watoto wawili ambaye ni mkazi wa Iringa, alibahatika kuibuka mshindi katika droo ya Shinda Nyumba iliyochezeshwa Juni mwaka jana, lakini kwa kuwa ni mjasiriamali huko Iringa anakoishi, aliamua kuipangisha nyumba hiyo na fedha anazopata, zinamsaidia kulipia karo za watoto wake wawili, mmoja akiwa kidato cha pili na mwingine akisoma chekechea.

Mr. Shinda Nyumba akikabidhi zawadi ya flana kwa Maneno Mohammed.

 

Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Jimmy Haroub, wakati akizungumza na wakazi wa Kiwangwa alisema kuwa huu ni wakati muafaka wa wasomaji wote waliokata kuponi zao kuziwasilisha kwa mawakala wao nchi nzima.

 

Victoria Kolombani akijaza kuponi.

“Nyumba siyo kitu kidogo, kila mtu angetamani kumiliki nyumba jijini Dar es Salaam, sasa hii ni fursa adimu ambayo haikulazimu kuwa na mamilioni ya kujenga au kununua, ni kiasi cha kwenda kwa muuza magazeti yeyote, popote alipo Tanzania na kujipatia mojawapo ya magazeti yetu ili ujiweke katika nafasi nzuri ya kuwa mmoja wa wamiliki wa nyumba bora nchini,” alisema Jimmy.

 

Nyumba hiyo ambayo kama ile ya kwanza imejengwa Dar es Salaam, itakuwa ni ya kisasa ikiwa na samani zote ndani yake, kiasi cha kumfanya mshindi kuingia na begi lake tu ili kuanza maisha. Bahati nasibu hii ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Premier Bet.

NA RICHARD BUKOS | GPL

Breaking News: Rais Magufuli Agoma Kusaini Waliohukumiwa Kunyongwa

Leave A Reply