The House of Favourite Newspapers

SHINDA NYUMBA YATIKISA TAIFA

Wasomaji wakichangamkia Gazeti la Championi.

 

WAKATI klabu za soka mahasimu wa jadi nchini za Simba na Yanga zikichuana jana katika mchezo wa Ngao ya Hisani, mashabiki wengi walijitokeza kupata kuponi pamoja na zawadi mbalimbali kutoka kwa timu ya promosheni ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inayokaribia kufanya droo kubwa.

 

Wasomaji wakichangamkia Gazeti la Championi.

Mashabiki hao walinunua kwa wingi Gazeti la Championi na Risasi Mchanganyiko ambayo yalikuwa na kuponi za Bahati Nasibu hiyo ya Shinda Nyumba, ikiwa ni pamoja na kujipatia zawadi mbalimbali zikiwemo fulana, kofia na vitu vingine vidogovidogo.

 

Wasomaji wa Championi wakiwa katika picha na Mr. Shinda Nyumba.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inafanyika baada ya ile ya kwanza kufanyika Juni mwaka jana ambapo Nelly Mwangosi, mama wa watoto wawili ambaye ni mkazi wa Iringa, alibahatika kuibuka mshindi katika droo kubwa ya mwisho.

 

Msomaji akijaza kuponi.

Kwa sasa, Nelly ambaye ni mjasiriamali, ameipangisha nyumba hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam wakati yeye akiendelea na maisha huko Iringa anakoishi.

 

Msomaji akijaza kuponi ya Shinda Nyumba.

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, aliwataka wasomaji wa magazeti ya Ijumaa, Championi, Uwazi, Amani, Ijumaa Wikienda na Risasi, kujipatia kuponi zao wakati huu shindano likielekea ukingoni, kwani bahati siku zote haina mwenyewe.

 

Wasomaji wakiwa bize kujaza kuponi ya Sinda Nyumba.

“Tunaelekea ukingoni, watu wapate kuponi zao zilizopo katika magazeti yote ya Global kisha watume moja kwa moja kwa sanduku la barua lililoonyeshwa au wazilete ofisini kwetu kwa wale walioko Dar, lakini wale wa mikoani, wawaone mawakala wetu ambao wako kila wilaya na mikoa ili ziweze kusafirishwa kwa ajili ya droo kubwa.

 

Wasomaji wakiwa katika picha ya pamoja na Mr. Shinda Nyumba.

“Nyumba siyo kitu kidogo, kila mtu angetamani kumiliki nyumba jijini Dar es Salaam, sasa hii ni fursa adimu ambayo haikulazimu kuwa na mamilioni ya kujenga au kununua, ni kiasi cha kwenda kwa muuza magazeti yeyote, popote alipo Tanzania na kujipatia mojawapo ya magazeti yetu ili ujiweke katika nafasi nzuri ya kuwa mmoja wa wamiliki wa nyumba bora nchini,” alisema Mkanda.

Nyumba hiyo ambayo kama ile ya kwanza imejengwa Dar es Salaam, itakuwa ni ya kisasa ikiwa na samani zote ndani yake, kiasi cha kumfanya mshindi kuingia na begi lake tu ili kuanza maisha.

Bahati Nasibu hii ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Premier Bet.

NA MWANDISHI WETU

 

Breaking News: Chadema Wafunguka Kukamatwa kwa Lissu na Bulaya

Comments are closed.