The House of Favourite Newspapers

British Airways Lafuta Safari 100

SHIRIKA  la ndege la Uingereza, British Airways,  leo Agosti 7, 2019 limefuta safari za ndege 100 na nyingine 300 kukaa hewani zaidi ya saa moja baada ya mfumo wa komputa kushindwa kufanya kazi kwa ndege zinazotumia viwanja vya ndege  Heathrow na Gatwick kwa mujibu wa habari zilizotolewa na website ya shirika hilo.

 

Shirika hilo linalomilikiwa na International Airlines Group (ICAGY), limetoa taarifa kwamba kwa sasa wanaendelea kutumia mfumo wa kizamani  kutoa huduma kwa wateja wake huku wakigoma kutoa sababu ya tatizo la  mfumo wake wa komputa kushindwa kufanya kazi.

 

Msemaji wa shirika hilo amesema abiria ambao safari zimeahirishwa wanatakiwa kukata tiketi tena Agosti 8 mpaka Agosti 13 mwezi huu.

 

Ndege zilizochelewa kutua  Heathrow zilikuwa zinatoka Los Angeles, New York, Philadelphia, Pittsburgh, Charlotte, Nashville na Miami.

 

Si mara ya kwanza kwa shirika hilo kuahirisha safari zake, kwani  ilishatokea 2017 ambapo safari za ndege zinazotoka Heathrow na Gatwick baada ya mfumo wa komputa wa abiria zilishindwa kufanya kazi na kukwamisha abiria zaidi ya  75,000.

 

Comments are closed.