The House of Favourite Newspapers

Betika litabaki kuwa juu

WASOMAJI wa Gazeti la BETIKA katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, wameonekana kuwa walikuwa na shauku kubwa sana ya kulisubiri gazeti hilo lianzishwe.

Hiyo imetokana na namna ambavyo wamekuwa wakilisifia kila likiingia mtaani kwamba limekuwa mkombozi wao kwa kipindi cha muda mfupi hasa kwenye masuala ya kubeti.

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, linatolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na huingia mtaani kila Jumatano huku leo Agosti 7, ikiwa ni toleo la 26.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi tofauti duniani.

Leo Jumatano, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, ilitembelea maeneo ya Vingunguti, Kiembe Mbuzi, Kwa Ally Mboa, Kijiwe Samli, Abiola na maeneo mengine ya Jiji Dar es Salaam na kukutana na wasomaji mbalimbali wa Gazeti la Betika.

Mmoja wa wasomaji aliyepata nafasi ya kulizungumzia Betika, alisema: “Hivi sasa sipati shida sana wakati wa kubeti tofauti na zamani ambapo nilipokuwa nikibeti, huwa nikipata shida sana.

“Betika limenifanya niwe na uwezo wa kubeti kwa urahisi, kiukweli tangu lianzishe limenisaidia sana, siyo mimi tu bali hata rafiki zangu. Ama kweli Betika litabaki kuwa juu.”

Naye Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema heshima ya Betika imeendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo hasa kwa kuwa bei yao ni nafuu na imewavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kuleta matangazo yao.

“Hili ni gazeti la bure, linawahusu watu wazima kuanzia umri wa miaka 18, linatolewa bure kabisa kwa wauza magazeti wote nchini.

“Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao yetu ya kijamii katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

“Kupitia hayo matangazo ambayo yapo ndani ya Betika, msomaji akijipatia nakala yake anapata faida mara mbili, kwanza kufahamu odds mbalimbali za kubet, lakini pia kufahamu mambo mbalimbali yanayowahusu watangazaji wetu hao.

“Wanaohitaji kutangaza nasi tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au barua pepe [email protected], bei zetu ni nafuu, muhusika anaweza kufika Sinza Mori, Dar, kwenye jengo letu la Global Group,” alisema.

Comments are closed.