The House of Favourite Newspapers

Shoga, Ona Aibu ‘Kidumu’ Kumfanyia Usafi Mumeo

0

Couple-in-BedNajua nikisema sana nitaonekana nina mdomo wakati kila kiumbe hapa duniani kina mdomo, lakini kwa vile kuwapasha ndiyo ‘hobi’ yangu acha niwachane ‘live’ simuogopi mtu hasa wewe mwenye hila ya kwapa kunuka bila kidonda.

Mambo mengine unaweza kuona kama ni kichekesho, kwa vile mimi nyani mzee niliyeishi muda mrefu na kukutana na shuruba za porini siwezi kuliacha hivi hivi likapita kwani aibu hii inashusha heshima ya ndoa.

Siku hizo nyumba ndogo siyo siri tena, sasa hivi asilimia tisini ya wana ndoa lazima wanakuwa na vidumu nyumba ndogo.

Wenye ndoa tumekuwa ndiyo hasa tukiwalazimisha waume zetu wazitafute raha nje baada ya kukosekana ndani. Nilielezea wiki jana jinsi wanawake tunaposhindwa kujitambua, tukiachika tunasema tumerogwa, kumbe wachawi ni sisi wenyewe.

Juzi kuna shoga yangu wa karibu alinieleza kitu ambacho kwa kweli kilinihuzunisha sana. Shoga yangu mwenyewe mwingi wa habari anawapenda waume za watu ambao anasema wanajua kutunza si waongo kama walio singo. Kama kawaida alimtia mikononi mume wa mtu aliyejipendekeza, baada ya kukutana naye alichokutana nacho kilimfanya amshushe thamani mkewe na kumuona ni mwanamke kimaumbile lakini hana hulka ya kike.

Anasema baada ya yule mwanaume kukaa mkao wa kula, alichokutana nacho kinatia kichefuchefu. Mwanaume kichaka kimeota unaweza kusuka tatu kichwa, si huko tu, hata kwapani nako ndiko usiseme mpaka zimebadilika rangi na kuwa za njano. Ikabidi kabla ya mchezo aingie kazini kumfanyia usafi mume huyo wa mtu.

Najiuliza hayo mapenzi na mkewe wanafanya gizani na hata kama gizani huwa hakutani na hali hiyo tete?

Kibaya hata aliporudi nyumbani mkewe hakuona mabadiliko yoyote, najiuliza, anayekaa naye kweli anamjua vizuri mumewe?

Kweli huyo mwanamke alipitia mafunzo ya wanawake kumjua mwanaume anatakiwa afanyiwe nini?

Siku nilipooneshwa huyo mwanamke mwenye mume anavyojipenda utashangaa. Yupo smati kila kona ya mwili, amechafuka kwa midhahabu lakini kumtunza mumewe sifuri. Nilikuwa na wasiwasi hata yeye shamba lake limejaa majani yaliyokosa mtunzaji.

Nyumba ndogo imekuwa kubwa kutokana na kila kitu kinachomhusu mwanaume anakifanya yeye, wewe upo tu unabakia na sifa ya kuolewa lakini mke jina.

Kwa mtindo huu wanawake wachache watabakia katika ndoa zao, jamani hata kwa hili mtasema nachonga sana, tuliache hivihivi lipite ili umpe nafasi nyumba ndogo! Hivi kweli wewe mwanamke unamwachia mumeo na mikucha na minywele kibao hutaki kumnyoa mpaka aende nyumba ndogo? Aaah!

Sipendi miye aibu hii imkute mwanamke mwenzangu, hebu mtunze mumeo apendeze, huyo anayetaka kukuibia akose kazi ya kufanya.

Siyo akidondokea nyumba ndogo utasikia jamani kweli mkeo hakupendi, hata kucha anashibdwa kukukata?

Hebu basi tunapowafanyia usafi waume zetu tusiishie kufua tu, bali ni kumfanyia kila kitu kuanzia kucha hadi kumnyoa kila kona ya mwili wake.

Unataka nani aguse mali zako jamani! Mdudu wa sikio hapendi rafiki, kwa kuamini moyo una nafasi moja ya upendo wengine mnakuwa matawi lakini shina huwa moja.

Kumbuka kwamba, kitendo cha kumfanyia usafi mumeo kinaonesha ni jinsi gani unavyompenda na kumjali jambo litakaloongeza mashamshamu ya mapenzi yenu.

Nina imani nimesomeka, ila kama unataka darasa zaidi kuhusu maisha ya ndoa usikose kuungana nami hapa wiki ijayo ili tupige stori.

Ni mimi Anti Nasra, Shangingi mstaafu.

Leave A Reply