The House of Favourite Newspapers

Shoga; ukichoka mwambie kistaarabu, usiseme hutaki!

0

Shoga yangu, natumai hali yako ni nzuri na unaendelea vizuri na pilika za maisha, kwa upande wangu Mungu ni mwema mambo yanakwenda vizuri.

Leo nataka kutoa darasa kuhusiana na lugha ambayo mama aliyechoshwa na kazi za nyumbani au ofisini anayopaswa kuitumia kwa mumewe aliyebanwa na njaa ya ‘chakula cha usiku.’

Nimeamua nizungumze nawe kuhusu mada hii kwa sababu tabia ya akina mama kuwakatalia waume zao kuwapa haki yao bila kutumia lugha ya kistaarabu imekuwa chanzo cha wababa kutafuta michepuko jambo ambalo ni hatari.

Shoga, ukweli ni kwamba akina mama wengi wanakuwa bize sana na malezi ya familia, kazi na mambo mengine kiasi wakati wa usiku baadhi huwa wanachoka na kutohitaji kuwa faragha na waume zao.

Kufanya hivyo ni kukosea kwa sababu ukimfanyia hivyo mara kadhaa tena kwa kusema hutaki, utamkwaza mumeo atakayeamua kutafuta mtu wa pembeni atakayekuwa anakata kiu yake.

Naelewa akina mama mnachoshwa sana na majukumu ya kila siku lakini lazima uwe na lugha ya kistaarabu ya kumpoza mumeo ambaye anakuhitaji mlicheze segere kwa sababu sidhani kama yupo mwanaume ambaye ukimweleza jinsi ulivyochoka atakulazimisha.

Naamini kama mumeo ni mwelewa, akifika nyumbani na kukuta rundo la nguo chafu lililokuwepo umefua, umefanya usafi wa nyumba, umepika na kuwahudumia vizuri watoto sidhani kama ukimwambia awe mpole chakula chake kipo atakula kesho atakataa!

Shoga, kikubwa hapo ni lugha tu ya kistaarabu lakini kama utajenga tabia ya kumwambia hutaki wallahi abillahi itakula kwako ni lazima atatafuta dogodogo wa kubembea naye kwa raha zao.

Je, utajisikiaje utakapogundua mumeo ana mchepuko ‘ulioutengeneza’ wewe? Jibu unalo!

Leave A Reply