The House of Favourite Newspapers

SHOO YA TWANGA USIKU WA KUAMKIA LEO USIPIME

Diouf akiwatambulisha vijana wapya katika bendi hiyo.

Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ usiku wa kuamkia jana Jumapili ilifanya onesho yake ndani ya Ukumbi wa The Jonz uliopo Magomeni Mwembe-Chai Jijini Dar ambapo hufanya makamuzi kila Jumamosi.

Bendi hiyo imeanza kujizolea tena umati wa mashabiki kwenye maonesho yake hali iliyoonekana kurudi kwenye ubora wake. Akizungumza na mtandao huu Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka alisema siri ya bendi hiyo kurudi kwenye ubora wake ni safu ya vijana wapya aliowaongeza kwenye kundi hilo.

Asha aliwataja vijana waliokuwa kwenye safu ya uimbaji kuwa ni pamoja na Zubeir, Fetty na Joshua, upande wa dram, Kirikuu na ngoma za tumba zinapigwa na mdada, Brightness. Vijana hao wataongozwa na wakongwe akiwemo, Msafiri Diouf, Kalala Junior, Chaz Baba, Jojoo Jumanne na wengineo.

Matukio katika Picha

HABARI: PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL    

Comments are closed.