Sibomana: Msiogope, Tunawapiga Kwao Botswana

KIUNGO mshambuliaji machachari na tegemeo hivi sasa wa Yanga Mnyarwanda, Patrick Sibomana amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaahidi ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers.

 

Mnyarwanda huyo ambaye ndiye mfungaji wa bao la kusawazisha la Yanga kwa njia ya penalti, aliitoa kauli hiyo mara baada ya mchezo huo kumalizika uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana kati ya Agosti 23-25, huko Botswana mara baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa awali.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Sibomana alisema kuwa Wanayanga wasiogopeshwe na matokeo waliyoyapata nyumbani huku akiahidi kupata matokeo ugenini.

 

Sibomana alisema katika mchezo huo kama wangekuwa makini wangefunga mabao zaidi ya mawili kutokana na nafasi walizozitengeneza na kushindwa kuzitumia vema katika kufunga mabao.

Aliongeza kuwa ana imani kocha wao Mkongomani, Mwinyi Zahera ameona makosa ambayo atayafanyia kazi ili kabla ya mchezo huo na kupata matokeo mazuri.

 

“Lolote linaweza kutokea katika kuelekea mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Rollers, kikubwa sisi tutaingia uwanjani kwa ajili ya kupata ushindi pekee ambacho ndiyo kitu cha umuhimu.

“Wapinzani siyo wabaya sana, lakini wanafungika kutokana na ubora wa timu yetu na kikubwa sisi tunakwenda Botswana kufuata ushindi na hilo linawezekana,” alisema Sibomana.

WILBERT MOLANDI NA SAID ALLY, Dar

Loading...

Toa comment