The House of Favourite Newspapers

Siki ya tufaha kwa fangasi wa kucha

0

Watu wengi wamekuwa wakishindwa kuvaa viatu kwa sababu ya fangasi wa ngozi na wakati mwingine fangasi wa kucha, sasa basi ili kuponya
fangasi wa kucha tumia tiba hii itakusaidia

Siki ya Tufaha  ‘Apple Cider Vinegar’
Nimeshaandika sana kuhusiana na siki hii, lakini imekuwa ikitibu mambo mengi na unapokwenda kutafuta dukani, hakikisha imeandikwa Apple Cider Vinegar ndio utakuwa umepata ninayoizungumzia.
Chukua kiasi kidogo cha siki ya tufaha inayolingana na maji kisha changanya vyote kwa pamoja, osha kucha zako au loweka miguu au mikono, kaa mpaka nusu saa ifike kisha toa, kama una tatizo siriasi tumia kila siku kisha kausha miguu yako, utaona unapona kwa siku chache.

Baking Soda
Wengi wameizoea kuchanganya kwenye maandazi, lakini pia inatibu magonjwa mengi na yenyewe ipo kwenye orodha ya tiba za fangasi wa kucha na harufu ya miguu. Chukua Baking Soda kidogo, changanya na Hydrogen Peroxide kidogo kisha paka kwenye kucha zako, acha kwa muda wa dakika 10 kisha osha kwa maji ya baridi.
Rudia mara mbili kwa wiki utaona matokeo, utapona harufu yote pia utajikuta umesahau shida ya fangasi wa kucha.

‘Listerine Mouthwash’
Bila shaka kila mtu anajua Mouthwash, huwa tunatumia kusukutua mdomoni ili kuondoa harufu mbaya na kuua bacteria, sasa hii inatumika kwenye kutibu hili tatizo la fangasi wa kucha, ili kutibu chukua Mouthwash kidogo uchanganye na siki nyeupe vyote vilingane, tumia kupaka miguu kisha acha kwa muda wa dakika 30 kisha osha.

Leave A Reply